Breaking News

Your Ad Spot

Apr 14, 2011

TANZANIA KUUZA TANI 50,000 ZA TUMBAKU IRAN: NYARANDU


SERIKALI inatarajiwa kufanikisha kuuza tani 50,000 za tumbaku nchini Iran kwa bei nzuri ikiwa ni sehemu ya kukuza kilimo nchini.
Mafanikio hayo yanatokana na ziara ya kutafuta soko nchini Iran, ya naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyarandu aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika kutafuta soko la zao hilo kufuatia wakulima kuzalisha kuwango kikubwa cha ziada.
Akizungumza jana jioni baada ya kurejea kutoka Iran Nyalandu alisema tumbaku itakayouzwa nchi Iran ni ile ambayo imekosa soko la ndani. 
 Alisema kwa mujibu wa wataalam, licha ya kuwa Tumbaku inayouzwa nchini Iran nyingi inatokea nchini Zimbabwe na China lakini inayozalishwa Tanzania ina ubora wa aina yake. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages