Breaking News

Your Ad Spot

Apr 29, 2011

JAJI MSTAAFU BARNABAS SAMATTA MGENI RASMI TUZO ZA EJAT; MZEE WA CHACHANDU DAILY NDANI YA KINYANG'ANYIRO


NA MWANDISHI WA CHACHANDU DAILY
MTAYARISHAJI wa Blogu ya Chachandu Daily, Bashir Nkoromo ni miongoni mwa wateule waliotinga katika fainali za kinyang'anyiro cha Tuzo za Umahiri katika Uandishi wa habari (EJAT) zitakazofanyika Mei 3, mwaka huu, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katika fainali hizo Nkoromo atawania tuzo ya Mpigapicha Bora kwa kuchuana vikali na mpigapicha wa magazeti ya Daily News, Robert Okanda kwa kuwa wameteuliwa hao wawili tu katika nafasi hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam,  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), John Mireny wakati akitangaza walioteuliuwa kuwania tuzo hiyo, alisema, mgeni rasmi katika sherehe ya utoaji tuzo atakuwa Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta.
Mireny alisema wateule wamepatikana baada ya jopo la majaji kupitia na kuchuja kazi 437 zilizowasilishwa na waandishi mbalimbali wa habari katika makundi 16 ya tuzo zinazoshindaniwa.
Alisema wakati Nkoromo na Okanda wakichuana kumpata mpigapicha bora, kwenye tuzo ya mchoraji bora wa katuni watamenyana Rashid Kagusa (Mwananchi), Nathan Mpangala (ITV) na Samuel Mwmkinga ( The Citizan).
 Mireny alisema habari za Utawala bora wanachuana Mbaraka Islam (Raia Mwema), Bernard James (The Citizen), Orton Kiishweko wa  Daily News na Mbazigwa Hassan,  Adeladius Makwega na Joseph Bura (TBC Taifa), Sima Bingileki (Manispaa ya Iringa ITV), Margareth Tengule (Star Tv) na Sam Mahela (ITV).
Katika Habari za Malaria, wanachuana Leon Bahati (Mwananchi),  Festo Sikagonamo (ITV), Lucas Liganga ( The Citizen) na Deogratius Mushi (Daily News) na kwa habari za Michezo na Utamaduni wakikwaana  Dorice Malima ( TBC1),  Masoud Masoud (TBC1) na  Malima Bundala.
Mireny alisema, Habari za wenye ulemavu, ni Victoria Patrick (TBC1),  Sabina Wandiba (Changamoto), Sam Mahela (ITV), Tumaini Msowoya (Mwananchi), Edwin Ndeketela (RFA-Radio France International/TBC FM na Tuma Dandi (Radio Mlimani) huku upande wa habari za Jinsia wakichuana Samwel Chamlomo (TBC 1), Stella Setumbi (TBC Taifa),  Dorcas Raymos (Chanel 10),  Florence Majani (Mwananchi), Sabrina Handing’oka (Uhuru FM) na Crace Kiondo (Zenj FM).
Habari za VVU na Ukimwi ni Amina Mollel (TBC1), Elesia Isabula (TBC Taifa), Orton Kiishweko (Daily News), Rose Mdami (Tumaini TV),  Jackson Jackon (Mlimani Radio), Martin Kuhanga (Radio Tumaini) na Doto Mnyadi (TBC 1), huku kwa habari za afya wakimenyana  Dorice Kaunda (TBC 1), Lilian Rugakingira (Mwananchi), Lina Denis (Chanel 10),  Aloycia Maneno (TBC Taifa),  Sheilla Sezzy (Mwananchi),  Elisia Isabula (TBC Taifa), Godfrey Nago (TBC1) na Sam Mahela (ITV).
Mireny alisema, upande wa habari za mazingira wanaochuana ni Godrey Nago (TBC1), Angel Akilimali (Uhuru FM), Felix Mwakyembe (Raia Mwema),  Mussa Twagilo (TBC Taifa),  Festo Sikagonamo (ITV), Salehe Masoud (Mlimani TV) na kwa habari za Uchumi na Biashara wakiwania  Cosmas Makongo (ITV), Emmanuel Chacha (Raia Mwema) na Ezekiel Kamanga ( Baraka FM ya Mbeya).
Habari za elimu, watachuana  Bilal Abdul-Aziz (The Guardian), Adeladius Makwega (TBC Taifa), Agness Tuniga ( TBC1), Happy Severine Mollel (Nipashe), Pius Ntiga (Uhuru FM) na Malinganya Charahani (Star TV) na tuzo ya habari za watoto  ni  Gervas Hubile (TBC Taifa), Angelo Mwoleka (Star Tv) na Victoria Patrick (TBC Taifa).
Mireny alisema, tuzo za Habari za Sayansi na Tknolojia,  Kazi  na Mahusiano sehemu za kazi na habari za mawasiliano hazikupata wasindani kutokana na kazi zilizopelekwa kushindaniwa kutokidi viwango.
Alisema, wateule sita waliomo katika makundi, Mwoleko, Masoud Masoud, Kiishweko, Kiondo, Raymos na kuhanga  wameteuliwa kuwa wanawania pekee wa nafsi ya mshindi wa jumla.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages