.

TWIGA STARS YATINGA FAINALI MICHUANO YA ALL AFRICA GAMES

Apr 15, 2011

Na Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake Tanzania Twiga Stars  (pichani) imefuzu fainali za  All  Africa Games inayotarajia kufanyika Septemba 3-18 mwaka huu, jijini Maputo baada ya Sudan kujitoa katika mchezo wa mchujo uliotakiwa kuchezwa Aprili 30 jijini Khartoum.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Angetile  Osiah alisema wamepokea taarifa kutoka shirikisho la soka Afrika (CAF) kuhusu kujitoa kwa Sudan.

Osiah alisema baada ya kujitoa Tanzania inajiandaa na fainali hizo ambapo awali walipangiwa na Uganda wakajitoa sambamba na Kenya pia.

“Ni wakati wa kujiapanga ipasavyo kwa sababu, inaonekana upinzani ni mdogo katika timu zinazoshiriki mashindano hayo,” alisema Osiah.

Aidha Osiah alisema kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa alishatangaza kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo na ilikuwa imeshaanza mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa.

“Unajua ukanda wa Afrika Mashariki na Kati tuna nafasi kubwa katika mashindano ya wanawake, hivyo ni nafasi ya kujivunia katika hilo,” alisema Osiah.

1 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª