KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imezindua rasmi kuanza kwa mashindano ya mchezo wa Pool kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini mwaka 2011.
Akizungumza na Waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, leo, Meneja wa bia hiyo, Oscar Shelukindo alisema TBL imeongeza sehemu ya udhamini wake katika mchezo huo kwa kuongeza idadi ya mikoa na vyuo vikuu kutoka mkoa mmoja wa Dar es Salaam pekee, mwaka jana hadi kufikia minane.
Shelukindo alisema, katika mashindano hayo ambayo mwaka jana, kilishinda Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka huu itahusishwa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha ambapo fainali kitaifa zitafanyika mkoani Dodoma mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Alisema, maandalizi ya mashindano katika ngazi za mikoa yamekamilika na yataanza na mikoa ya Morni Morogoro na Dodoma ambapo mjini Morogoro fainali ya hatua hiyo itafanyika Jumamosi, Mei 7, katika ukumbi wa DDC na mkoani Dodoma ni Jumapili katika ukumbi wa Royal.
Shelukindo alisema kuhusu zawadi mwaka huu ngazi ya mkoa na kitaifa zimetengwa jumla ya Sh. milioni 18.6 hatua ambayo alisema italeta changamoto katika mcheo huo kwa vyuo hivyo.
Alitaja mchanganuo wa zawadi za mikoa kuwa ni Mshindi wa kwanza (Sh. 500,000), Wapili (Sh. 300,000), mshindi wa tatu Sh. 200,000 na wa nne sh. 50,000 huku na wachezaji mmoja mmoja mshindi atapata sh. 100,000 na mshindi wa pili kati yao sh. 50,000.
Shelukindo alisema, kwa ngazi ya Taifa mshindi wa kwanza ni sh. milioni 2, wapili sh. milioni 1.5 na mshindi wa tatu sh. 1.3, huku mshindi wa nne akipata sh. milioni moja na washindi wa kwanza hadi wa tano hadi wa nane watapata kifuajasho sh. 500,000 kila chuo.
Pia upande wa mchezaji mmoja mmoja ngazi hiyo ya Taifa mshindi wa kwanza atapata sh. 300,000, wapili sh. 200,000 na watatu 150,000, wakati wanne atajipatia sh. 100,000.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269