Mtayarishaji Mkuu wa Blogu hii, ambaye ni mpigapicha wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Bashir Nkoromo, ameng'ara katika Tuzo ya Umahiri ya Uandishi wa Habari (EJAT) kwa mwaka 2010.
Nkoromo aliibuka mshindi wa picha bora dhidi ya Mpigapicha wa magazeti ya Daily News na Habari Leo, Robert Okanda, na kukabidhiwa tuzo, cheti na zawadi ya kamera.
Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Mhariri wa Habari wa Uhuru FM, Pius Ntiga, alipata Tuzo ya Elimu akimshinda Adeladius Makwega wa TBC Taifa.
Akishukuru baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Nkoromo alisema kwamba ushindi wake haumaanishi kuwa yeye ni bora zaidi ya wapigapicha wengine katika vyombo vya habari, bali picha aliyoipiga ambayo imempatia ushindi ndiyo ilikuwa bora.
Wadau mbalimbali wa sekta ya habari walihudhuria hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa, Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta.
Tuzo nyingine kadhaa zilikwenda kwa waandishi wa habari, watangazaji wa redio, televisheni na wachoraji wa katuni wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumza kweye hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanja,alisema utozji tuzo hizo umefikiwa baada ya kupata wateule 76, kupitia na kuchuja kazi 437 zilizowasilishwa na waandishi mbalimbali wa habari katika makundi 16 ya tuzo zinazoshindaniwa.
Mtia Chachandu za habari Mkuu wa Blogu hii, Bashir Nkoromo akiwa na tuzo na zawadi ya Kamera aliyotuzwa kwa kuibuka mpigapicha bora wa tuzo za EJAT
Tuzo ya cheti
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269