Breaking News

Your Ad Spot

May 15, 2011

NAPE, MARTHA MLATA WAPAGAWISHA KIMZIKI ITIGI

Nape na Martha Mlata wakiwajibika kwenye mkutanao huo
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Singida, Martha Mlata, juzi walipagawisha wananchi baada ya kupanda jukwaani na bendi ya Paradise Singers iliyokuwa ikitumbuiza kwenye mkutano wa kutambulisha wajumbe wa Sekretarieti ya CCM uliofanyika katika mji mdogo wa Itingi mkoani Singida.
      Baada ya msafara wa Wajumbe hao wa sekretarieti ya CCM kuwasili kwenye uwanja wa mkutano, bendi hiyo iliporomosha muziki wa mapokezi na ghafla, Nape alipanda jukwaani na kuchukua gita la besi na kuaza kulicharaza kwa madaha.
      Huhu Nape akiendelea kuonyesha umahiri wake katika kucharaza ala hiyo, Martha naye alimuunga mkono kwa kupanda jukwaani na kushika kinasa sauti cha mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo na kuanza kuimba bila kukosea mpangilio wa wimbo uliokuwa ukiendelea.
      Kwa zaidi ya dakika 10, ambazo Nape na Martha walishiriki kutumbuiza na bendi hiyo, wananchi na mashabiki wa muziki walionyesha kupagawa kwa kucheza kila mmoja alipo huku wakishangilia.
     Mingoni mwa waliojumuika kucheza ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Juma Abdallah na mwenyeji wao, Mbunge wa Manyoni Magharibi John Luwanji.
    "Hongereni sana bendi ya Paradise Singers, kwa weli mmejipatia mpiga gita mahiri Nape, huyu ni mwanamuziki wa kimataifa", alisema Chiligati baada ya burudani ya muziki kumalizika.
     Mbali na kupiga gita, Nape aliwakumbusha mbali viongozi na wananchi waliohudhuria mkutano huo, baada ya kuimba wimbo wa  kumsifu baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere na kuhimiza ualendo, wakati Chiligati alipokuwa  akikabidhi kadi kwa wanachama wapya  57 wa CCM.
      Wimbo huo uliwakuna wengi hasa wale wa enzi za Mwalimu, kwa kuwa miongoni mwa waliouimba enzi hizo ni Marehemu Brigedia mstaafu, Moses Nnauye baba ya Nape.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages