Maafisa wa Libya wamesema raia 15- wakiwemo watoto watatu- wameuawa katika shambulio lililofanywa na majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya NATO kwenye jengo magharibi mwa mji mkuu, Tripoli.
Siku ya Jumapili, Nato ilisema kushindwa kufanya kazi kwa silaha huenda ndio iliyosababisha mauaji ya raia katika shambulio la awali mjini Tripoli.
Mhariri wa Mashariki ya Kati wa BBC Jeremy Bowen alipelekwa kuona mabaki ya eneo la makazi ya Khweildy al-Hamidy, mwanachama wa kituo cha mapinduzi ya Libya, ndani ya mtandao wa serikali.
Maafisa wa Libya walimwambia roketi nane zilifanya mashambulio makali kwenye takriban saa 10 au 11 Jumatatu asubuhi. BBC SWAHILO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269