Breaking News

Your Ad Spot

Jun 12, 2011

MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA BAJETI KUENDELEA KESHO

NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MKUTANO wa nne wa bunge la bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/2012 utaendelea kesho mjini hapa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo wabunge kujadili mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano (2011/2012 -2015/2016.
Mpango huo wa kwanza wa maendeleo ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni mjini Dodoma na kisha wabunge kupewa semina juu ya mpango huo kabla ya kupata fursa ya kuanza kuujadili kesho na kesho.
Mpango huo wenye lengo la kuweka vipaumbele vitano vya maendeleo ikiwemo nishati, miundombinu ikiwemo reli, barabara, bandari, kilimo, viwanda, rasilimali watu na kuimarisha teknolojia ya habari na mawasiliano, utaanza kutekelezwa mwaka huu wa fedha na jumla ya sh.trilioni 42.5 zitahitajika kutumika kwa miaka mitano ikiwa ni sawa na zaidi ya sh.trilioni nane kwa mwaka.
Katika kikao hicho cha nne kitachoendelea Juni 15 hadi Juni 21 mwaka huu, wabunge wapata fursa ya kujadili bajeti ya serikali iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Mstafa Mkulo, bajeti ambayo inaelezwa na wadau wengi kwamba imegusa maeneo muhimu yenye tija kwa mwananchi wa kada ya chini

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages