Breaking News

Your Ad Spot

Jun 14, 2011

TAMASHA MAAMLUM LA WANAMICHEZO NA WASANII WALIOWAHI KUSOMA MAKONGO SEC KUFANYIKA JUMAMOSI HII

Na Mwandishi WetuTAMASHA maalum linalowahusisha wanamichezo na wasanii waliowahi kusoma shule ya Sekondari Makongo ‘Makongo Day Bonanza’linatarajiwa kufanyika jumamosi ya juni 18 katika viwanja vya Leader’s Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa tamasha hilo Boniface PAwasa alisema lengo la tamasha ni kuwakutanisha pamoja wanafunzi hao na wa sasa, sambamba na kuhamasisha kuendeleza vipaji walivyonavyo.

Alisema,tamasha hiulo pia lina lengo la kuwahamasisha wanafunzo toka shule mbalimbali kujali na kuithamini michezo pamoja n asana nyingine kutokana na ukweli kwamba tasnia hiyo kwa sasa imeweza kutoa ajira kwa vijana.

Pawasa aliongeza kuwa kupitia tamasha hilo kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka itakayohusisha wachezaji nguli wa zamani waliosoma shuleni hapo watakaokipiga na Yanga, huku kwa upande wa netiboli watapepetana na Bongo Movies.

Aliongeza kuwa pamoja na michezo hiyo kutakuwa na burudani toka kwa wasanii mbalimbali waliowahi kusoma Makongo pamoja na waliopo wakiwemo Dogo Janja, Mc Babu Ayoub, Seki, Bambo, Jose Mara, Kalala Junior na wengineo.

“Pia tumezialika shule mbalimbali kushiriki katika tamasha hilo zikiwemo Jangwani, Tambaza, Jitegemee, Tegete, Hazina International School, Kipingu Sports Academy na nyinginezo ambapo kiingilio kitakuwa sh.2000”, Alisema.

Baadhi ya wachezaji waliowahi kusoma makongo ni pamoja na JUma Kaseja, Mussa Mgosi, Nico Nyagawa, Jerry Tegete, Haruna Moshi, Yahaya Akilimali, Kandole Justine, Aron Nyanda, Ali Mayai, Muhaji Kampala, Mohamed Banka, Adam Matunga, Jemedary Said, MAjuto Komu, Aman Simba, Ngawina Ngawina na wengineo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages