Breaking News

Your Ad Spot

Jun 16, 2011

TANZANIA YASIFIWA KWA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA MAMA NA MTOTO

Rais wa Baraza Kuu la 65 la Umoja wa Mataifa, Bw. Joseph Deiss akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro kufungua majadiliano  kuhusu  Maendeleo. Mkazo ukiwa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia ( MDGs) hususani lengo namba 4 na 5 yanayohusu afya ya mama na mtoto. katika mazungumzo yake, Naibu Katibu Mkuu pamoja na mambo mengine, ameyahimiza mataifa kuwekeza katika huduma za afya  hasa kwa mama na mtoto kwakuwa  kuna manufaa makubwa na ni chachu katika  kunasukuma mbele ajenda za maendeleo.
-----------------------------------------------------------------------------
Na Mwandishi Maalum,New York
Imeelezwa kuwa  Tanzania chini ya uongozi wa Rais Jakaya  Mrisho Kikwete  imekuwa  nchi ya kupigiwa mfano  , katika utoaji na uboreshaji wa huduma ya afya  kwa  mama na mtoto.
Ni kutokana na juhudi hizo,  Tanzania imetajwa kama  mdau muhimu  katika  utekelezaji wa  Mkakati   wa  Kimataifa  kuhusu  afya  ya mama na mtoto.
Hayo yameelezwa na  Bw. Joseph Deiss, Rais wa Baraza Kuu la 65 la Umoja wa Mataifa, wakati  alipokuwa  akimkaribisha   Mhe.  Juma Duni Haji, Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  kuzungumza katika  mjadala kuhusu Maendeleo uliofanyika siku ya jumanne Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Mhe. Juma Duni Haji alikuwa miongoni wa jopo la wazungumzaji   waliojadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia na Uwajibikaji, hususani utekelezaji   malengo  namba  4 na 5   yanayohusu afya ya mama na mtoto.
Majadiliano  hayo yalifunguliwana  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Dkt. Asha-Rose Migiro.
“ Tanzania ni mdau muhimu sana katika utekelezaji wa Mkakati wa Kimataifa kuhusu  Afya ya Mama na  Mtoto. Rais wake ni Mwenyekiti mwenza wa  kamisheni ya  habari na uwajibikaji katika masuala yanayohusu afya ya mama na mtoto. Tanzania inapiga hatua kubwa na nzuri na umejiwekea malengo  na mikakati mbalimbali katika eneo hilo” akasema Bw. Deiss.
Akasema kuwa  Tanzania imefanya vizuri katika  usambazaji wa  huduma za afya, utoaji wa chanjo za kuzuia maradhi mbalimbali kwa wanawake wajawazito na watoto  chini ya miaka mitano.
Aidha  ameongeza kuwa Tanzania , imejitahidi sana kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, na inatoa huduma za kinga ya  maambukizi ya virusi vinavyosababisha ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto huku ikiendelea na jitihada za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Mbali ya Mhe. Juma Duni  Haji wengine waliokuwa kwenye jopo hilo la mzunguko wa kwanza katika majadiliano hayo ni  pamoja na   Mhe. Gilles Richard, Naibu Balozi wa Canada katika Umoja wa Mataifa, Bw. Babatunde Osotimehin, Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA. Bi Donna J. Hrinak,  Makamu wa Rais kuhusu sera na masuala ya serikali  (PepsiCo) na  Ms. Nyaradzayi Gumbonzvanda,  Katibu Mkuu , World YWCA.
Akichangia majadiliano hayo, Waziri wa Afya Juma Duni Haji, alisema   anajisikia fahari kubwa kutamka  kwamba Tanzania  ilikuwa katika  mwelekeo sahihi wa kufikia utekelezaji wa baadhi ya  Malengo ya Maendeleo ya Milenia ( MDGs).
Waziri aliwaeleza washiriki wa majadiliano hayo, hatua mbambali ambazo serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar, zimetekeleza wa malengo namba 4 na tano katika utoaji wa huduma za afya ya  mama na mtoto, ingawa bado kuna changamoto kadhaa.
Kwa mfano alieleza kuwa hivi sasa huduma za afya zimesogezwa karibu zaidi  na wananchi ili kuwapunguzia  wananchi  na hasa wanawake mwendo mrefu wa kufuata huduma hizo.
Akasisitiza kuwa chanjo za magonjwa mbalimbali zimekuwa zikitolewa kwa wakati na kwa gharama nafuu, huku akielezea kuwa matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu kumesaidia sana kupunguza siyo tu vifo vinavyosababishwa na malaria, bali  kumetokomeza kabisa ugonjwa huo  Zanzibar.
 Aidha amesema  kumekuwa na ongezeko la ajira kwa wataalamu wa masuala ya afya.  Huku akisema ndoa za umri mdogo hasa kwa  Tanzania Visiwani bado ni tatizo
Awali akifungua majadiliano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro amerejea tena wito wake wakuzitaka serikali kuwekeza  zaidi katika huduma za afya na mama na mtoto.
Akasema uwekezaji katika afya ya mama na mtoto unalipa, kwa sababu mama akiwa na afya nzuri atazaa mtoto mwenye afya nzuri na ambaye hatimaye atakuja kuwa kiongozi mzuri.
Akasema kuwa katika dunia ambayo hivi sasa inakabiliwa na changamoto nyingi, ni rahisi sana kwa baadhi ya makundi ya watu na hasa wale wanaoishi katika mazingira magumu kusahauliwa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages