Breaking News

Your Ad Spot

Jun 16, 2011

ZANZIBAR WATAKA SHERIA YA KUDHIBITI UVAAJI NGUO ZINAZOCHAFUA HALI YA HEWA KIMAADILI

Serikali imeombwa kuangalia uwezekano wa kutunga sheria za mavazi ili kusaidia kuwadhibiti wale wote wanaojihusisha na uuzaji na uvaaji wa nguo zisizozingatia maadili, silka na utamaduni wa Mzazibari.
Taarifa ya Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imesema kuwa ombi hilo limetolewa na wananchi shehia mbalimbali wakati wa ziara ya Maafisa wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi za kuwaelimisha wananchi juu ya Polisi jamii na Ukamataji salama wa watuhumiwa. 
 Wakizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Nyerere eneo la Sebleni mjini Zanzibar, Viongozi hao wamesema kuwa nguo fupi na zinazobana maungo kwa mabinti na zile za kuvaliwa chini ya makalio kwa vijana wa kiume zimekuwa zikiwazalilisha na kupotosha maadili ya wakazi wa visiwa hivyo.

Akijibu hoja hizo, Msaidizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar SP Mukini Mohamme Ali, amesema kuwa pamoja na ombi hilo lakini ipo haja ya wazazi na walezi kudhibiti nyendo, liugha chafu na tabia mbaya zinzofanywa na watoto wao wakiwemo mabinti na wavulana ili wasipotoke na kuipotosha jamii.

Naye Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Mjini Magharibi SSP Ahamada Abdallah Khamis, amewakumbusha wananchi kutochukua sheria mkononi kwa kuwaadhibu watuhumiwa na hata kuwaua kwa vipigo wanapowakamata.

Mkuu huyo wa Upelelezi amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni kumezuka tabia ya wananchi kuwapiga, kuwatesa na hata kuwaua watu wanaowatuhumu kufanya makosa ya kihalifu kwenye jamii zao.

Maafisa hao wakiongozwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, tayari wameshazitembelea shehia 53 kati 74 zilizopo katika mkoa hua kwa lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya mpango wa ulinzi shirikishi na Ukamataji Salama wa wahalifu. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages