Breaking News

Your Ad Spot

Jun 15, 2011

VODACOM YAICHANGIA CCBRT SH. MILIONI 40

Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba katikati akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba  wa shilingi Milioni 40, zilizotolewa na Vodacom Foundation kwa CCBRT kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto katika hospitali mpya ya CCBRT Boabab.Kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa  CCBRT  Erwin Telemans,watatu toka kushoto Meneja Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans kushoto ,Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba wakisaini makubaliano ya Vodacom Foundation kuchangia shilingi Milioni 40 za ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto kwenye Hospitali mpya ya CCBRT Boabab itakayojengwa jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia katikati Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na kulia Meneja Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas
  
Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (kulia) Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule wakimwangalia  Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans (kushoto) akisoma mkataba wa makabadhiano ya shilingi Milioni Arobaini kutoka Vodacom zitakazotumika katika ujenzi wa jengo la wanawake na watoto katika Hospitali ya CCBRT Baobab itakayojengwa  jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages