Breaking News

Your Ad Spot

Jul 29, 2011

AJALI YA BASI MOSHI, CCM YATOA POLE KWA MAJERUHI


Katibu wa CCC mkoa wa Kilimanjaro,Steven
Kazidi (kulia), akipatamaelezo kutoka kwa muuguzi mkuu wa
Hospital ya Rufaa ya KCMC, Redempta Mamseri 
 kuhusu maendeleo  ya majeruhi waliolazwa katika hosiptal hiyo
 kufuatia ajali ya basi la LimSafari iliyotokea juzi joni nje
kidogo ya manispaa ya Moshi.
 CHAMA  cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Kilimanjaro,kimetoa pole kwa majeruhi wa ajali
ya  Basi iliyotokea juzi jioni katika bara bara ya kibosho road nje kidogo ya
Manispaa ya Moshi.

Katika ajali hiyo iliyohusisha basi la Lim Safari lenye namba za usajili T489BJR
na roli la mizigo aina ya Bitisubishi Fuso lenye namba za usajili T884BFJ
likiendeshwa na dereva wake Sifael Kaaya,watu 11 walifariki papo hapo wakiwamo
madereva wote wa magari hayo mawili.

Wote waliofariki ukiondoa madereva hao,ni vibarua waliokuwa  wakirejea makwao
huko machame wilaya ya Hai wakitoka kuvuna kahawa katika shamba la kahawa la
Kilimanjaro Plantretion Ltd ambalo lipo eneo la Kibosho wilaya ya Moshi
Vijijini.

Mashuda wa ajli hiyo walisema dereva wa basi hilo,alikuwa amelewa na hakuweza
kusikia kilio cha abiria wake waliomtaka apunguze mwendo.

Akitoa pole jana katika Hosiptal ya rufaa ya KCMC baada ya kutembelea majeruhi
wa ajli hiyo,katibu wa CCm mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi,alisema ajali hiyo
inatoa funzo kwa mamlaka husika kuwajibika katika kusimamia sheria za usalama
barabarani.

Katibu huyo alisema kuwa,aajli nyingi zinatokea kutokana na uzembe wa madereva
na kutaka jitihada zifanywe na vyombo husika kutoa adhabu kali kwa madereva
wanaosababisha ajali.

Alisema Chama cha Mapindizi CCM kimeguswa na ajali hiyo na katika kuonesha kwa
vitendo,CCM ilitoa msaada wa sh,600,000 na kati ya hizo sh,300,000 zilitolewa na
Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Manispaa ya moshi .

Msaada huo aliutoa kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya uuguzi katika Hospital
hiyo ya KCMC Redempta Mamseri aliyepokea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospital
hiyo,Moshi Ntabae.

Kazidi ambaye alitembelea Idara ya upasuaji katika hospital hiyo na kuzungumza
na baadhi ya majeruhi ,alifuatana na katibu wake msaidizi,Habas Mwijuki, Kamanda
ya UVCCM Manispaa ya Moshi Agrrey Marealle  na Katibu wa CCM Manispaa ya
Moshi,Amos Shimba.

Kwa upande wake kamanda wa UVCCM Manispaa ya Moshi,Agrrey Marealle ,alitioa wito
kwa serikali kuona umhimu wa ajali za barabarani kuongezwa katika orodha ya
majanga ya kitaifa   pamoja na kuweka sheria kali za kudhibiti uzembe kwa
madereva.

Aidha Marealle alishauri serikali kuboresha elimu ya madereva kwa kutoa elimu
kila mara juu ya sheria za usalama barabarani,kudhibiti mianya ya rushwa ikiwamo
biashara ya leseni bandia na pia kuwa na utaratibu wa madereva kurudia majaribia
ya udereva(driving test) mara kwa mara .

alishauri pia kuweka mkazo katika kuwadhibiti madereva wanaoendesha vyombo vya
moto huku wakiwa wamelewa,kupunguza safari za usiku pamoja na kutoa muda wa
kupumzika kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo bila hivyo taifa
litaendelea kupoteza nguvu kazi hasa vijana.

"Bila hivyo tutaendelea kupoteza watu hususani vijana ambao ndiyo raslimali kuu
ya nchi,kampeni hii inahitaji ushirikiano kati ya polisi na serikali,vyama vya
siasa,vyombo vya habari,madhehebu ya dini na jamii kwa ujumla"alisema Marealle.

katibu wa ccm mkoa wa kilimanjaro,Steven Kazidi,akimpa pole Bi.Esimend Parimina
ambaye amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya KCMC baada ya kujeruhiwa jicho lake
la kulia katika ajali ya basi la Lim Safari iliyotokea juzi jioni eneo la
kibosho road nje  kidogo ya Manispa ya Moshi,watu 11 walipoteza maisha yao na
wengine 26 kujeruhiwa vibaya. 
Katibu wa CCC mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi(mwenye suti kulia)akipata
maelezo kutoka kwa muuguzi mkuu wa Hospital ya Rufaa ya KCMC,Redempta
Mamseri(kushoto  aliyevaa gauni la kijani) kuhusu maendeleo  ya majeruhi
waliolazwa katika hosiptal hiyo kufuatia ajali ya basi la LimSafari iliyotokea
juzi joni nje kidogo ya manispaa ya moshi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages