Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais, Jakaya Kikwete alipowaili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, katika sherehe ya mkesha wa kuzaliwa kwa TANU. Kulia ni Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abdulrahman Kinana.
Wana-CCM wakiserebuka nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba wakati wa mkesha huo wa kuzaliwa kwa TANU usiku wa kuamkia leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiliza king'ora kuashiria kuzaliwa kwa TANU, kwenye Ofisi Ndogo ya makao makuu ya CCM Lulumba. Shughuli hiyo ilifanyika katika jengo ilimozaliwa TANU 7/7/1954
Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakiondoka Lulumba, kwenda viwanja vya Mnazi Mmoja kuendelea na mkesha wa kuzaliwa TANU
Rais Kikwete akimsalimia Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, aliposalimia wana-CCM mbalimbali kabla ya kuondoka Lumumba
Wananchi waliofurika viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye sherehe hizo
Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akiwa na Makamu wake, Pius Msekwa, Katibu Mkuu Wilson Mukama na mkewe Mama Kikwete baada ya kuwasili viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Wapili kushoto Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita na kulia ni mlezi wa CCM mkoa huo, Abdulrahman Kinana.
Kikwete, Msekwa na Mukama wakijadili jambo wakati wa sherehe hiyo
Mamia ya wana-CCM na wananchi kwa jumla waliohudhuria sherehe hizo.
Mamia ya watu upande wa lango la kuingia viwanja vya Mnazi Mmoja
Burudani zilikuwepo, Marlow akitumbuiza
Halafu Ze Top In Town au TID naye akafanya mavituz yake kama hivi
Nape akaona haitoshi, akapanda jukwaani na kucharaza gita zito la bass, kuwapa tafu Vijana jazz
Kisha akazikung'uta tumba
Mama Salma Kikwete akamkubali kuwa kweli Nape ni mwanamuziki mahiri, akaenda kumtuza nteze kibao
Baada ya burudani, Kikwete akiambatana na muasisi wa mstari wa mbele wa TANU kati ya wawili waliopo hai Costantine Milinga, kwenda kuliza king'ora ilipotimu saa sita kamili usiku wa kuamkia leo
Rais Kikwete na Mzee Milinga wakishirikiana kubonyesha king'ora hicho
Wakati akiendelea kubonyeza king'ora, mafataki nayo yalikuwa yaiendelea kuunguruma huku watu wakishangilia. Kushoto ni Nape, Mama Kikwete, Msekwa, Mukama na kulia ni Kinana wakishangilia
Baadhi ya fataki zilizorindima Mnazi mmoja
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisawiri jambo na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye katika sherehe hiyo
Nape na JK wakifurahia tukio hilo
Kikwete akizungumza jambo na Nape, Guninita na Msekwa
Kapteni Komba akiongoza kundi la TOT kuimba wimbo maalum wa kupongeza miaka 57 ya TANU
Rais Kikwete akaanza kuondoka uwanjani kwa kusalimia wadau na viongozi mbalimbali, hapa anamwaga Katibu wa UVCCM, Martine Shigella. Kushoto ni Mama Kikwete
Akamuag Nape
Akawaaga wadau mbalimbali kama hivi
Nape akatumia fursa hiyo kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwa nyakati tofauti baada ya Mwenyekiti, Rais Kikwete kuondoka. Hapa anazungumza na watangazaji wa Uhuru FM
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269