Breaking News

Your Ad Spot

Jul 28, 2011

MAREALLE AONYA JUU YA MAKUNDI CCM MOSHI


Kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi mjini  Aggrey Marealle
akihutubia  katika uzinduzi wa baraza kuu  la CM  Manispaa ya
Moshi  kuzindua rasmi baraza hilo mjini Moshi. Kulia ni Katibu
wa  CCM wilaya ya Moshi mjini  Amosi Shimba na kushoto ni
Mwenyekiti  wa Makamanda wa Vijana Moshi Mjini
Alhaji Omari Shamba.

MFUMO rika , makundi ndani ya chama  na baadhi ya viongozi kushindwa kusimamia serikali kwa kutatua kero za wananchi ni miongoni mwa sababu kuu zilizochangia  Chama cha Mapinduzi (CCM) kushindwa  nafasi ya ubunge katika jimbo la Moshi Mjini katika  uchaguzi mkuu uliopita.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Vijana wa moshi mjini  kupitia CCM Aggrey Marealle katika hafla ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa baraza la vijana wa jimbo hilo uliofanyika katika chuo cha maendeleo ya wananchi Msinga kilichopo kata ya Kibosho wilayani Moshi vijijini.

Marealle alisema pamoja na chama chao kufanya kampeni na maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanakomboa jimbo la moshi bado jimbo hilo lilibaki mikononi mwa wapinzani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mfumo rika ambao vijana wengi walipigia kura chama cha CHADEMA wakiamini watapata maisha bora zaidi.

Alisema sababu nyingine ni baadhi ya viongozi kushindwa kuwajibika katika nafasi zao na hivyo wananchi kuona serikali haiwajali na kuamua kupiga kura kwa chama kingine wakiamini watapata maendeleo bora zaidi.

Kwa mujibu wa kamanda huyo wa vijana rushwa ndani ya chama na nje ya chama ni sababu nyingine iliyochangia chama hicho kushindwa kwani baadhi ya wananchama walikua CCM mchana na usiku kuwa chama cha upinzani huku wakitoa siri za chama ili wapewe kitu kidogo.

Mbali na rushwa pia tatizo la utoaji kadi kiholela kwa kuamini wote
wanaochukua kadi ni wananchama ilikigarimu kwa watu wasiofaa kupiga ura wakati wa kura za maoni na hivyo kusababisha makundi ndani ya chama hususan kipindi cha uchaguzi mkuu.

Alisema uratibu wa kura za maoni katika jimbo la moshi mjini uligawa chama kwa kiasi kikubwa na kuwafanya wagombea wengine kuwa upande wa pili licha ya wao kuonyesha kuwa chuki za kura zimeisha.

Kutokana na hali hiyo Marealle alishauri uongozi wa chama hicho ngazi za juu kuona umuhimu wa kuacha nafasi kati ya muda wa kura za maoni na uchaguzi ili wale watakaoshindwa kwenye kura za maoni wawe wamevunja makundi kukinusuru chama.

Katika hatua nyingine Marealle aliwataka vijana wa chama hicho kufuata kanuni na taratibu za chama na kuhakikisha wanatangaza chama hicho kwa vijana wenzao ili nao waweze kujiunga na kuinua upya chama hicho.

Alisema chama hicho kina ugonjwa wa woga,kwa kila mmoja kuogopa kumkemea mwenzake hata kama atamwona akikisaliti chama jambo ambalo limeendelea kukitafuna chama kama mchwa ambapo aliwataka vijana kuhakikisha wanakua mstari wa mbele kupinga tabia hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages