Breaking News

Your Ad Spot

Jul 13, 2011

NBC YAKABIDHIA TUZO YA 'HESHIMA' YA UFANYAKAZI BORA

NA MWANDISHI WETU
JUMLA ya wafanyakazi kumi na tatu wa Benki ya NBC Tanzania wamekabidhiwa zawadi mbalimbali kutokana na utendaji kazi wao uliotukuka katika sherehe zilizofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Kwa kawaida kila mwaka NBC hutoa tuzo katika tukio lijulikanalo kama ‘Heshima Awards’ ikiwa ni kama ishara ya Menejimenti ya NBC kuridhishwa na utendaji kazi wa wafanyakazi wa benki hiyo kwa mwaka wa fedha uliopita.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunukia wafanyakazi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru alisema kuwa hiyo ilikuwa ni mara ya nne kwa wafanyakazi kutunukiwa Heshima Awards.
“Kila mwaka huwa tunaangalia vipengele vinne katika tuzo zetu navyo ni Jamii; Wateja; Uongozi/Wafanyakazi na Fedha/Wanahisa,” alisema Mafuru.
Washindi walikabidhiwa vyeti, fedha taslimu huku majina yao yakipelekwa kushindanishwa kwenye tuzo za benki mama ya NBC, ABSA.

“Wafayakazi wote wa NBC walishiriki kuwachagua washindi hawa kwa kujaza fomu maalumu na kutoa sababu za kuwachagua wastakaoshindania tuzo za fedha, shaba na dhahabu. Kisha fomu hizo hukabidhiwa kwenye Kamati Maalumu ya Heshima Awards kwa shughuli za kukamilisha zoezi lenyewe,” alisema Mafuru.

Washindi wa mwaka huu waliopata tuzo za dhahabu ni Rajab Maalim( tawi la Zanzibar), Salma Yatera(tawi la Moshi),  Jacqueline Sindano(tawi la Corporate, Dar-es-Salaam), na Margareth Touwa(tawi la Mwanza) na zawadi kubwa kabisa  ya hafla hiyo ya mshindi wa MD iliangukia kwa Anna Leon Moshi kutoka tawi la NBC Babati.

“Hakika tukio hili linahamasisha sana. Linaonyesha jinsi uongozi wa NBC unavyowajali wafanyakazi wake,” mmoja wa waalikwa alisema baada ya washindi kutunukiwa.
Washindi siku zote ni wale waliofanya jambo kubwa litakalowashawishi wajumbe wa kamati na wafanyakazi wote wa benki kuamini kuwa muhusika anapaswa kuzawadiwa.
Miongoni mwa mifano iliyowazi ni tukio la Desemba mwaka jana wakati Luciana Kipiko alipopokea hundi yenye thamani ya Sh 46,750,000 iliyochukulewa kwenye Tawi la Corporate Dar es Salaam na kupelekwa tawi la Dodoma.
Baada ya kuishitukia, Luciana aliituma kwa fax Dar es Salaam ili ithibitishwe na hata ilipothibitishwa bado Luciana aliitilia shaka na kuamua kumpigia simu Meneja wa Corpaorate, na ikagundulika kuwa ilikuwa imeghushiwa.
“Kitu kama hicho kilitokea kwa mfanyakazi wa Tawi la Mwanza, Margareth Touwa aliyeishitukia hundi ya Sh 221,000,000 iliyopelekwa na Mnada Enterprises Machi mwaka jana na kesi bado iko mahakamani.
“Hivyo ni muhimu kama si lazima kwa NBC kuthamini michango na kujitolea kwa dhati kunakofanywa na wafanyakazi wa aina hii,” alisema MD.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC  wakiwa katika picha ya
pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Lawrence Mafuru (wa sita
kushoto mstari wa nyuma) katika hafla ya kila mwaka ambayo benki hiyo
hukabidhi tuzo mbalimbali kwa wafanyakazi wake bora maarufu kama
‘Heshima Awards’ jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages