Breaking News

Your Ad Spot

Jul 13, 2011

KUJIVUA GAMBA: ROSTAM AZIZI ATEMA UNEC NA UBUNGE

Habari za kweli tulizopata kutoka Igunga mkoani Tabora, zimethibitisha kwamba Mbunge wa Igunga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kupitia mkoa wa Tabora, Rostam Aziz  (pichani) leo ametangaza kujivua nafasi hizo za uongozi. Kufuiatia hatua hiyo bila shaka ametimiza maamuzi ya kujivua gamba ndani ya CCM, yaliyopitishwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika Aprili mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo kibao, kikao hicho kilivunja Sekretarieti yake yote na Kamati Kuu na kuingiza viongozi wapya, na pia kuazimia kwamba wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kutajwa sana, wapime wenyewe na kujiondoa kwenye ngazi za maamuzi za Chama. Wengine wanaotuhumiwa ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Chenge.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages