Breaking News

Your Ad Spot

Jul 31, 2011

RAIS KIKWETE KUFUNGUA MAONYESHO YA NANE NANE KESHO

Rais Kikwete
 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kesho, Agosti Mosi, 2011, atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Wiki ya Sherehe za Nane Nane na Maonyesho ya Kilimo mwaka huu kwenye Uwanja wa Maonyesho ya Kilimo wa Nzuguni, Dodoma.
Shughuli kuu za Mheshimiwa Rais katika ufunguzi huo itakuwa ni kufungua Maonyesho ya Kilimo ya Nane Nane kwa hotuba rasmi na baadaye kutembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho hayo.
Hotuba hiyo ya kesho itakuwa badala ya Hotuba ya Mwisho wa Mwezi wa Julai ambayo ilikuwa itolewe jioni ya leo, Jumapili, Julai 31, 2011 lakini haitatolewa kwa sababu ujumbe na maudhi yake yatakuwemo katika hotuba ya kesho.
Mheshimiwa Rais tayari yuko mjini Dodoma tangu jana, Jumamosi, Julai 30, 2011 kwa vikao vya Chama cha Mapinduzi ambacho yeye ni Mwenyekiti wake wa taifa.
Mara baada ya kuwasili jana, Rais Kikwete aliendesha Kikao cha Kamati ya Maadili na leo amekuwa anaendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages