Kwa upande wa klabu za Ligi Kuu, usajili wao unaanzia kwa timu za pili (U20), hivyo kwanza zinatakiwa kukabidhi usajili wa timu hizo na baadaye za timu zao za kwanza (senior). Klabu zote za Ligi Kuu tayari zina passwords zao kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji wa kigeni.
Dirisha dogo la usajili litafunguliwa tena Novemba 1 hadi 30 mwaka huu. Tunazikumbusha timu zote za Ligi Kuu kuwasilisha majina ya viwanja ambavyo zitatumia kwa ajili ya ligi hiyo ambayo itaanza Agosti 20 mwaka huu.
Klabu ambazo zimewasilisha maombi ya viwanja ambavyo zitatumia ni Mtibwa Sugar (Manungu), Azam (Chamazi), Ruvu Shooting Stars (Mlandizi), Coastal Union (Mkwakwani), Toto Africans (CCM Kirumba), Oljoro JKT (Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta), Polisi Tanzania (Jamhuri, Dodoma) na Kagera Sugar (Kaitaba).
Klabu ambazo bado hazijawasilisha viwanja vyao ni Yanga, Simba, Moro United, Villa Squad, JKT Ruvu na African Lyon. Timu hizo zinatakiwa kutuma majina ya viwanja vyao haraka, kwani kabla ya kuruhusiwa kutumika ni lazima vithibitishwe na Kurugenzi ya Ufundi ya TFF.
U23 v SHELISHELI
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23, Jamhuri Kihwelo ametangaza orodha ya wachezaji 21 kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Shelisheli.
Mechi hizo mbili zitachezwa Julai 27 na 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.
Wachezaji hao ni Juma Abdul (Mtibwa Sugar), Himid Mao (Azam), Babu Ally (Morani), Shabani Kado (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Godfrey Wambura (Simba), Jabir Aziz (Azam), Seif Juma (Ilala), Khamis Mcha (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Jackson Wandwi (Azam).
Wengine ni Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Thomas Ulimwengu (Humbarg SV, Ujerumani), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Mohamed Soud (Toto Africans), Jamal Mnyate (Azam), Awadh Juma (Moro United), Salum Kanoni (Simba), Salum Telela (Yanga), Samuel Ngasa (African Lyon) na George Mtemahanji (Modeva FC, Italia).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269