Hoteli ya kifahari ya Singita Grumeti Reserves iliyoko Serengeti Tanzania imekuwa hoteli ya kwanza kwa ubora kati ya hoteli 100 bora za utalii duniani, gazeti maarufu kwa mambo ya utalii nchini Marekani la Travel and Leisure limetangaza.
Kwa mujibu wa gazeti hilo ambalo linaaminika sana duniani katika masuala ya utalii, Singita Grumeti Reserves inayoendesha loji za Sasakwa,Sabora na Farufaru zilizoko Magharibi ya Serengeti zimepewa alama 98.44 zikifuatiwa na hoteli ndugu za Singita Sabi Sand inayoendesha hoteli za Ebony, Boulders na Castleton zilizoko Afrika ya Kusini kwa kupata alama 97.95.
Hoteli zingine za Tanzania zilizong’ara ni pamoja na Kirawira iliyopata alama 96.71 ikiwa katika nafasi ya tisa, Serengeti Migration yenye alama 96.50 ikiwa katika nafasi ya kumi na Ngorongoro Crater iliyoko nafasi ya 18 ikiwa na alama 95.14.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kupata nafasi hiyo na kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Singita Grumeti Reserves alisema amefurahishwa sana kwa kupewa heshima hiyo ambayo pia ni changamoto kwao.
“Ni furaha kubwa sana kupata tuzo kama hiyo inayotambulika duniani, lakini pia ni mwanya mzuri kwa sekta ya utalii nchini ambayo naamini itapanua uwigo wa biashara ya kujaza watalii Tanzania. Hii ni matunda ya kazi ya pamoja ya mimi na wenzangu wote hapa kazini,” alieleza Mr Ledger.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Travel and Leisure orodha kamaili ya washindi wa Nyanja zote za utalii kwa 2011 ni Hoteli bora duniani ni Singita Grumeti Reserves; mji bora ni Bangkok; kisiwa bora ni Santorini kilichopo Greece; meli bora kubwa ya utalii ni Crystal Cruises na meli bora ndogo ya utalii ni Seabourne.
Meli bora ya mtoni ni Tauck; shirika bora ya ndege la kimataifa ni Singapore Airlines; shirika bora la ndege kwa safari za ndani ya nchi ni Virgin America; tour operator bora ni Micato Safaris; kampuni bora ya magari ya kukodi ni Zipcar; Spa bora ni Rancho la Puerta Fitness Resort and spa Tecete-Mexico na Sofitel Queenstown and Spa ya New Zealand.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269