Breaking News

Your Ad Spot

Jul 12, 2011

LOWASSA AKUTANA NA MUFTI, AMKABIDHI MILIONI 13 ZA MRADI WA SHULE YA SEKONDARI KIGAMBONI

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akimkabidhi fuba la sh. milioni 13, Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa Shaaban bin Simba, kwa ajili ya kusaidia shule ya sekondari la Edward Lowassa iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Mufti ambaye ni mlezi wa shule hiyo, Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi mwakani kwa kuanzia na wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza, na kwamba fedha hizo zitatumika kukamilisha baadhi ya mambo ya shule hiyo ikiwemo kujenga bweni la watoto 30, choo cha shule, kisima cha maji na shule itajihusisha zaidi kusomesha yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kulia ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo. 
Lowassa akimsindikiza Mufti wakati akiondoka baada ya hafla ya kumkabidhi fedha hizo, iliyofanyika Ofisini kwake, Mikocheni, Dar es Salaam. 
Wakiagana  baada ya shughuli hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages