Breaking News

Your Ad Spot

Aug 28, 2011

KAMATI KUU YA CCM KUWAJADILI KESHO WANACHAMA WAKE WALIOOMBA KUGOMBEA UBUNGE IGUNGA

NA MWANDISHI WETU
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, inakutana kesho mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa na CCM leo imesema kikao hicho kitafanyika mchana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, pale mtaa wea  Lumumba.

"Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama  agenda za mkutano huo ni kupokea na kujadili taarifa ya maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi mdogo jimbo la Igunga ambayo itaenda sambamba na kujadili mapendekezo ya wana CCM wanaoomba kuteuliwa na CCM kugombea jimbo hilo", imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema, pia  Kamati Kuu itapokea na kujadili mapendekezo ya wana CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya meya wa manispaa ya Songea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  Mukama amesema Kamati Kuu haitaishia hapo, mbali na hayo itajipa uwanja wa kujadiliu na kuamua kuhusu masuala mengine mbalimbali ya ndani ya Chama.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages