Washiriki 30 wa Vodacom Miss Tanzania leo (jana) walichuana vikali katika siku ya michezo ya Miss Tanzania iliyofanyika kwenye ufukwe wa bahari wa Hoteli ya Jangwani See Breeze iliyopo Mbezi Kilongawima jijini Dar es Salaam.
Wakiadhimisha siku hiyo washiriki hao wa shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo nchini walichuana kwenye michezo mbalimbali ikiwemo Volleball, kuruka kamba, kukimbia na magunia, mbio za vijiti, kuvuta kamba na michezo mingine ya kuvutia.
Akizungumzia siku hiyo Meneja Uhusiano na Habari kwenye Mtandao Matina Nkrulu alisema lengo la siku hiyo ni kuwaunganisha warembo pamoja wakiwa tayari kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya shindano hilo.
Akifafanua Nkurlu alisema kwamba mbali ya kuwaunganisha michezo pia imesaidia kuibua vipaji vya warembo hao mbali na fani ya urembo wanayojihusisha nayo.
“Tukiwa kwenye siku ya michezo ya Vodacom Miss Tanzania warembo wameonesha vipaji vyao vya kimichezo jambo lililowafanya pia kuendelea kuwa pamoja kama ilivyo tasnia hiyo kwamba inawaunganisha watu wote bila kujali dini rangi au kabila.
Kwa wake mrembo Glory Lory amesema siku hiyo ni ya faida kwao kwani wameweza kujifunza michezo mbalimbali ambayo walikuwa hawajawahi hata kuipitia.
Akifafanua Glory alisema mbali ya kujenga afya pia wamepanua mtazamo wa kiakili kwani ni moja ya fani zinazoenda kushindaniwa katika shindano la Miss World kwa atakayebahatika kuliwakilisha taifa.
“Michezo ni moja ya vipengele kwenye shindano la urembo la dunia, hivyo kwa atakayebahatika atafanya vizuri kwani mazoezi haya yamempika tayari kwa kwenda kushiriki michuano hiyo ya urembo ya dunia.
Nae Mkuu wa kitengo cha Itifaki wa Kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye alisema ari waliyonayo warembo inaonesha utayari wao katika kuliwakilisha taifa katika medani za kimataifa.
“Mmejionea wenyewe washiriki wetu walivyochuana katika michezo mbalimbali katika kuadhimisha siku ya michezo kwa warembo. Hili tu linadhihirisha kwamba shindano la mwaka huu litakuwa na changamoto kubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita,” alisema Makoye.
Tayari washiriki hao wanaoishi ndani ya jumba la Vodacom wameanza kupigiwa kura na watazamaji wa vituo vya televisheni Star tv na Clouds TV baada ya maisha yao ndani ya nyumba kuoneshwa moja kwa moja na vituo hivyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269