Nape Nnauye (wapili kulia) akikata keki maalum iliyoandaliwa katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne ambao ni wanachama wa Jumuia ya wanafunzi wakatoliki Tanzania (TYCS) Kanda ya Kimala, kuchangisha fedha za kuimarisha jumuia hiyo, leo Kimara, Dar es Salaam. Kulia ni Mlezi wa TYCS Kimala, Padri Zengo. Watatu kulia ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi Kinondonbu, Stanley Mkandawile |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinatambua mchango wa Makanisa katika kujenga maadili ya vijana.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne, wanachama wa Jumuia ya Wanafunzi Wakakatoliki Tanzania (TYCS) Kanda ya Kimara, Dar Salaam.
"Mchango unaotolewa na madhehebu ya dini mkiwemo Wakatoliki hapa nchini, kwa kweli ni mkubwa sana na ndio unaochangia kwa kiasi kikubwa kujenga uadilifu kwa vijana na Wananchi kwa jumla", alisena Nape na kuongeza. "Uadilifu unaotolewa na dini huwajenga vijana na wananchi kwa jumla kumweka mbele Mungu wao katika kila jambo na hivyo kuwa sababu kubwa ya kuwa waadilifu kuliko wale wanaofanya mambo yao bila kutanguliza Mungu".
"Hata viongozi wetu wanapokuwa katika upokeaji rushwa hufanya hivyo kutokana na kutokuwa na hofu ya Mungu kwa kuwa wakati wakifanya hivyo kujiona yupo yeye na mtoa rushwa tu Mungu hayupo nao, tofauti na mwadilifu ambaye huogopa kupokea au kutoa rushwa kwa kuwa moja ya mambo yanayomzuia ni kutambua kuwa popote alipo Mungu yupo", alisema Nape.
Nape alisema hatua ya dini kuwapatia vijana malezi ya Kimungu kunawafanya kuwa binadamu wa kwa sababu binadamu asiye na malezi ya Kimungu hahofii chochote anapotenda jambo na kwa hiyo huwa hana tofauti na mnyama yeyote kama simba au bweha.
Alisema, malezi ya kimungu huwafanya watu kuwa waadilifu zaidi ya wale ambao kufanya uadilifu kwa kuhofia sheria za serikali na kwamba hata yakiwepo magereza mengi kiasi gani bado wasio na uadilifu unaotokana na malezi ya Kimungu wengi hawaogopi.
Nape aliwataka wahitimu hao na vijana kwa jumla kuwa na malengo wanapotaka kufikia mafanikio mazuri katika maisha yao na baada ya kuweka malengo kuyalinda kwa kukwepa yale yanayoweza kusababisha wasifikie malengo hayo.
"Kwa mfano ukiweka lengo la kufaulu mtihani lazima ujitahidi kukwepa vishawishi vinavyoweza kukufanya usifikie lengo hilo kama utoro shuleni, kulala badala ya kujisomea na kupenda starehe", alisema.
Aliwataka kujiepusha na mazungumzo mabaya akisema mazungumzo ya aina hiyo huwa chanzo cha kuharibu tabia njema ya kijana.
Nape aliwataka vijana kuwa makini wanapotembelea mitandao katika konpyuta na simu zao kwa kuwa licha ya ubora wa mawasiliano kwa njia hiyo lakini mna taarifa nyingi za uongo na upotoshaji wa maisha malisi.
Katika sherehe hiyo Nape alikabidhi vyeti kwa wanafunzi zaidi ya 300 na kukata keki maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuendeleza Umoja wa TYCS Kanda ya Kimara ambapo kabla ya kuondoks zilikusanywa sh. 500,000 zikiwemo 100,000 alizochangia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269