Breaking News

Your Ad Spot

Aug 29, 2011

LOWASSA ALIMWAGIA KKKT MAMILIONI YA FEDHA

NA MWANDISHI WETU KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Mwenge, Dar es Salaam, limevuna zaidi ya sh. milioni 119 zikiwemo sh. milioni 30.7 zilizochangwa na Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowassa katika harambee ya  kuchangisha fedha za kumalizia ujenzi wa kanisa hilo.
   "Mimi sina cha kikubwa cha kuchangia hapa, niseme tu kwamba nimekuja kuwazindulia harambee hii nanyi mtachangia kwa kadri ya nguvu zetu, lakini kuongoza ni kuonyesha njia kwa hiyo mimi nikisaidiwa na familia na marafiki zangu nitachangia sh. milioni 30.7", alisema Lowassa.
          Baada ya kutamka hivyo na kukabidhi kibunda hicho cha minoti kwa Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo Kanda ya Mashariki na Pwani, Geoge Fupe, harambee hiyo iliyofanyika kwa watu kuchangia papo hapo na kunadiwa vitu mbalimbali, ilmalizika kwa kuingiza sh. 119,562,300
.       Mapema katika risala, Mchungaji  Luhuvilo Sigala alisema, ili kumalizia ujenzi wa kanisa hilo zilikuwa zinahitajika sh. milioni 94 na kwamba hadi sasa kanisa hilo limeshajengwa kwa asilimia zaidi ya 80.
        Baadhi ya vitu vilivyonadiwa na Lowassa ambnaye alaifuatana na Mkewe, Regina Lowassa, ni mbuzi watano waliotolewa na waumini, mchele, sukari na mikungu ya ndizi.
        Akizungumza katika misa kabla ya harambee hiyo, Fupe aliwataka waumini wa Kikristo na hususan wa KKKT kuhakikisha wanawalea watoto wao katika mazingira ya kupenda dini ili kuweza kupatikana waumini wa baadae.
       Fupe alisema kujenga makanisa bora bila  kuwalea watoto katika malezi hayo hakutakuwa na faida yoyote kwa sababu baada ya miaka ijayo  yatabakia makanisa mengi yasiyo na waumini.
      "kuna nchi nilitembelea hivi karibuni nikashangaa kuona makanisa makubwa makubwa, nilipohudhuria misa na kuombwa kuiendesha nilishangaa kukuta kanisa kubwa lakini ndani mna waumini wachache mno" alisema Fupe na kuongeza.
       "Nikauliza mbona kanisa ni kubwa mno tena la ghorofa lakini waumini wachache? nikaambiwa siku hizi waumini hawaji kanisani na sababu kubwa ni kwamba vijana wamenyimwa utamaduni wa kuabudu walipokuwa watoto", alisema.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages