Breaking News

Your Ad Spot

Aug 6, 2011

RAIS KIKWETE AFUTURU NA YATIMA IKULU


Rais Kikwete akimhudumia chakula
mmoja wa watoto yatima aliofuru nao Ikulu
Dar es Salaam ,jana.
                                                                    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa, Agosti 5, 2011, amewafuturisha watoto yatima kutoka vituo vya kulea watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi katika Mkoa wa Dar es Salaam.
             Watoto hao yatima wanakuwa kundi la kwanza la jamii kualikwa kwenye futari na Mheshimiwa Rais tokea kuanza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka huu,  Jumatatu wiki hii, Agosti Mosi.
Kiasi cha watoto 250 kutoka vikundi vinane vya yatima wameshiriki futari hiyo iliyomshirikisha pia Mama Salma Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.
Tofauti na jadi yake katika shughuli za kufuturisha, ambako kwa kawaida hazungumzi, Mheshimiwa Rais Kikwete ameamua kuzungumza na watoto hao. Akizungumza kwa ufupi kabisa, Mheshimiwa Rais amewashukuru watoto hao kwa kukubali mwaliko wake wa kuwataka washiriki pamoja katika futari akisema:
      “Nyie ndiyo mmefanikisha shughuli hii. Nawashukuru sana kuwa mmepata nafasi ya kuja kwa sababu shughuli ni watu.”
Rais Kikwete pia amewahakikishia watoto hao kuwa pamoja na kwamba wamepotelewa na wazazi wao, bado jamii inawatambua, inawajali na iko tayari kuwalea. 
Amesema: “Nataka mtambue kuwa sisi tunajua kuwa nyie mpo na tunataka mjue kuwa tunawajali na hata kama hamna wazazi, sisi wazazi wenu wengine tupo kwa ajili yenu.”
Amesisitiza Mheshimiwa Rais: “Napenda kuwahakikishieni kuwa tunawajali sana. Jamii ipo na inaendelea kuwajali na itaendeleza kuwatunza ili muishi maisha ya kawaida kabisa bila vikwazo vya msingi.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
06 Agosti, 2011
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimhudumia mmoja ya watoto yatima aliowaalika katika futari  ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.Rais Kikwete jana jioni alifuturu na baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam. 
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi kwa baadhi ya watoto yatima alofuturu nao jana jioni ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu zake za mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa baadhi ya watoto yatima aliowaalika ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni(picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages