Breaking News

Your Ad Spot

Aug 6, 2011

UCHAGUZI MDOGO IGUNGA KUFANYIKA OKTOBA 2, MWAKA HUU.


Aliyekuwa Mbunge wa Igunga (CCM)
Rostam Aziz
 Uchaguzi mdogo jimbo la Igunga utafanyika Oktoba 2, mwaka huu,  na uteuzi wa wagombea kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo utafanyika Septemba 6, NEC imesema.

Kaimu Mkurugenzi wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  Dk. Sisti Cariah amesema jijini Dar es Salaam, pia uchaguzi mdogo katika wa Udiwani katika kata 22 ambazo viti vyake vipo wazi utafanyika Septemba 22, mwaka huu. 
        Katika taarifa yake aliyosambaza kwa kwenye vyombo vya habari, Dk. Cariah alisema kampeni katika jimbo la Igunga zitaanza  Septemba 7 na kukamilika Oktoba Mosi, wakati kwa uchaguzi mdogo zitaanza Septemba 30 na kukamilika Oktoba 1.

Jimbo la Igunga limebaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz kuachia ngazi kutokana na kuhemewa na tuhuma za ufisadi kama alivyoeleza katika taarifa yeke wakati akitangaza kujiuzulu.

Mbali ya kuutema ubunge, Rostam aling'oka pia katika kiti cha Ujumbe wa NEC ya CCM, ikiwa ni kutekeleza mamuzi ya CCM kutaka wanaotuhumiwa kwa ufisadi wapime na kujitoa katika vikao vya maamuzi ya Chama.

Hata hivyo Rostam katika uamuzi wake baada ya kumwaga ugali wa U-NEC CCM akaamua umwaga na mboga ya Ubunge a jimbo hilo pengine kuifanya CCM isivune fedha za ruzuku kutoka jimbo hilo, licha ya kwamba amebaki kuwa mwana-CCM.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages