Breaking News

Your Ad Spot

Aug 1, 2011

ZOMBE AMSHUKIA LEMA,CHADEMA

*AAPA KUJINYONGA CHADEMA IKISHIKA DOLA !
Zombe akizungumza na waandishi wa habari leo
 Aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam, Abdalla Zombe, (kushoto)aliyeshinda kesi ya mauaji iliyokuwa ikimkabili , amemshukia Mbunge wa Arusha Mjini kwa  tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema kwa kuhoji kwa nini serikali ilimwacha huru katika kesi hiyo.

Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari, akiwa amefurika hasira Zombe alidai, Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani alitoa hoja hiyo wakati akisoma bajeti kivuli ya wizara hiyo Bungeni wiki iliyopita.

"Sijui aliandika nani hotuba ile, kwa vyovyote iliandikwa na tumu ya CHADEMA, lakini ninachotaka kusema hapa ni kwamba kwa Lema kutamka hoja kwamba kwa nini serikali imeniacha huru namshangaa sana, na ninapata picha kwamba Lema na viongozi wenzake wa CHADEMA hawajui haki za mwananchi zilizomo katika Katiba ya nchini", alisema huku akionyesha katiba.

"Na kama viongozi wenyewe wa CHADEMA ndio hawa, basi chama hicho kikishika uongozi wa nchi mimi ntajinyonga", alisema Zombe na kuwaacha midomo wazi waandishi kwa mshangao.

Alisema, ni uongo kusema aliachiwa huru na serikali katika kesi hiyo kwa sababu ni Mahakama ambayo inayo mamlaka kamili ya kikatiba ndiyo ilimwacha huru kwa mujibu sheria baada ya umuona hana hatia.

"Mimi sikuwachwa huru na serikali, bali niliachwa na mhimili wa Mahakama, na ndiyo sababu leo nimekuja hapa mahakama kuu kushughulikia kesi ya kuidai serikali inilipe fidia ya mamilioni ya fedha kwa kunifungulia mashtaka yale", alisema Zombe huku akionyesha hati za hukumu ya kesi ya mauaji iliyojuwa ikimkabili.

Alisema, angetarajia kuwa katika hotuba yake, Lema angehoji kwa nini wale waliotuhumiwa hasa kuua bado hawajakamatwa.

Akiendelea kumvaa Lema, Zombe alimshushia tuhuma nzoti mbunge huyo kwamba anamfahamu kuwa miongoni mwa wanamtandao waliokubuhu wa wizi wa magari mjini Arusha.
"Lema alikuwa mwanamtandao wa wizi wa magari kupeleka Kenya.. sijui kama amecha labda, lakini wakati nikiwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai, pale nilikuwa naletewa sana taarifa kuwa ni moja wa wanamtandao hatari wa wizi wa magari".

Zombe aliamua kuangusha bonge la press Conference nje ya lango kuu la mahakama kuu mjini Dar es Salaam, baada ya kutoka katika mahakama hiyo kushughukikia kesi ya madai dhisi ya serikali
kuhusiana na kei ya mauaji ambayo ameiponyoka na kuwachiwa huru.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages