Breaking News

Your Ad Spot

Sep 8, 2011

MKAPA ATUA IGUNGA


MWENYEKITI mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa aliwasili Igunga jana jioni kwa ajili ya kufungua kampeni za CCM za ubunge jimbo la Igunga, jumamosi hii.
" Nimewasili Igunga, wana-Igunga kazi ni moja, ni ushindi tu, alisema Mkapa akisalimia wananchi baada ya kupokewa katika kijiji cha Makomero kilometa nane kutoka mjini Igunga mkoani Tabora.

"Nashukuru sana kuona kwamba mara hii nimefika hapa Igunga kwa kupita barabara ya lami, mara ya mwisho nilipita kukiwa vumbi tu, jamani haya si maendeleo? alisema Mkapa huku akishangiliwa na wananchi.

Mkapa  (pichani) aliwataka wananchi wa Igunga kujitokeza kwa wingi Oktoba 2, mwaka huu kupiga kura na kuhakikisha wanampigia mgombea wa CCM Dk. Dalaly Peter Kafumu, akisema kufanya hivyo watakuwa wamechagua maendeleo.
"Lamsingi ni hilo mengine nitawaambia tutakapokutana katika mikutano ya kampeni, yapo mengi sana", alisema Mkapa.
Katika mapokezi hayo, Mkapa alipokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM, waliongozwa na Mratibu wa Kampeni za CCM jimboni humo, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, Katibu wa NEC , Oganaizesheni Asha Abdallah Juma na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassani Wakasuvi.
Baada ya kusalimia mwananchi msafara wa Mkapa ulikwenda mjini ukiwa na magari kadhaa, yaliyozungumwa na vijana waendesha pikipiki na baiskeli.
Kabla ya kuzindua kampeni za CCM, katika viwanja vya Kumbukumbu ya Samora mjini Igunga,leo Mkapa atakuwa na shughuli mbalimbali za kampeni na baada ya uzinduzi wa kampeni hizo ataendeleo na mikutano kesho yake. 
Mkapa akisalimiana na mgombea ubunge wa CCM jimbo la Igunga, Dk. Kafunu. Katikati ni Katibu wa
NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mraribu wa kampeni za CCM jimboni humo 
Msafara wa Mkapa ukienda mjini Igunga kutoka eneo la mapokezi 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages