Breaking News

Your Ad Spot

Sep 4, 2011

NAPE ATINGA IGUNGA, CHADEMA WATAHARUKI



Nape (wa pili kulia) akitoa pole kwa familia ya mtoto aliyefariki kwa kugongwa
na lori la mizigo mjini Igunga juzi alipokatiza barabara akitoka katika kundi
la wananchi waliokuwa wakisubiri msafara wa mgombea ubunge wa CCM

NNKOROMODAILY, IGUNGA
Katika hali ambayo haikutarajiwa Katibu wa NEC ya CCM, Nape Nnauye leo ametinga katika jimbo la Igunga mkoani Tabora na kuzusha taharuki kwa viongozi wa CHADEMA.
        Baada ya kuwasili, Nape alienda kutoa pole kwa familia ya mtoto Peter Ezekiel ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo, alipojaribu kukatiza barabara akitokea katika umati wa watu waliokuwa wakisubiri msafara wa mgombea wa CCM katika jimbo hilo.
       Kufuatia msiba huo, CCM ilisimamia taratibu zote hadi mazishi ambapo katika mazishi yaliyoyanyika juzi nye kidogo ya mji wa Igunga, CCM ilitoa rambirambi ya sh. milioni moja, huku CHADEMA ambao nao wameweka mgombea jimboni hapa wakitoa sh. 120,000.
      Nape aliwasili mjini Igunga saa sita mchana na kukatika safari yake kwenda moja kwa moja nyumbani kwa wazazi wa marehemu Ezekiel ambapo alitoa pole na kutoa ubani wa kiasi cha fedha ambacho hakupenda kukitaja.
     "Nisingependa kusema mengi hapa, lakini naomba niwaombe kuwa watulivu wakati huu mgumu kwa msiba wa mtoto wetu mpendwa. Hii ni mipango ya Mungu, nimeona nipite hapa kuwapa pole kwa kuwa nilipata habari za msiba huu", alisema Nape.
      Msemaji wa familia ya mtoto huyo, Joseph Mlewa alisema, familia hiyo imefarijika kwa namna CCM ilivyoshughulikia msiba mwanzo hadi mwisho na kwamba angeomba moyo huo uendelee kila inapopata fursa.
"Tangu msiba huu utokee wa Ezekiel CCM wametusaidia sana, wamesimamia hadi mwisho wa mazishi, tunasema asanteni sana CCM na tunawaombea kila la kheri kwa kila jambo mtakalofanya", alisema.
      Wakati Nape akiendelea kutoa pole Mratibu wa kampeni za CHADEMA Mwita Waitara alionekana akipiga doria kwa mbali kama aliyetaka kujua kilichokuwa kinaendelea na baadaye Nape alipotoka kutoa pole na kwenda kwenye baa moja jirani alikuwepo baunsa mmoja wa kuaminika wa chama hicho wa kutoka jijini Dar es Salaam ambao inaonekana alijaribu kufuatilia kwa karibu nyendo na kila kilichokuwa kikifanyika baada ya Nape kuwasili kwenye baa hiyo.
      Nape alizungumza na vijana kadhaa kwenye baa na kisha akaondoka na kupanda gari lake na kwenda hotelini. Haikuweza kufahamika ikiwa Nape atakuwepo jimboni hapa kwa muda mrefu au la ikizingatiwa kwamba kulikuwa na kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya vyombo vya habari kwamba hatakanyanga Igunga.
                                        HABARI ZAIDI KATIKA PICHA
Nape akimfariji Joseph Mlewa, msemaji wa familia ya mtoto marehemu Peter Ezekiel 
 Nape akimkabidhi ubani msemaji wa familia ya mtoto huyo
Mbali ya msiba wa mtoto aliyefariki kwa kugongwa na lori 
Nape akizungumza na wafanyabiashara katika soko la mjini Igunga mkoani Tabora leo 
Nape akimsalimia kada mmoja wa CCM aliyekutana naye ghafla katika soko hilo
Mfanyabiashara katika soko la Igunga ambaye kwenye banda lake ametundika bendera ya Chadema, akivalishwa kofia na Nape baada ya kuiomba kuvalishwa kofia hiyo ambayo Nape alifika akiwa ameivaa

1 comment:

  1. ha ha haaa, Nape umezamia tu hata hujaalikwa, wenzio wamekutoa nduki!

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages