Breaking News

Your Ad Spot

Sep 6, 2011

UCHAGUZI IGUNGA: MGOMBEA WA UMD ACHEMSHA!

Lazaro  siku alipochukua fomu zake
NA NKOROMO DAILY, IGUNGA
Wakati vyama vinane vimerejesha fomu zao kwa msimizi wa uchaguzi jimbo la Igunga chama cha UMD ambacho kilikuwa cha tisa kati ya vyama vyote vilivyochukua fomu kimechemsha baada ya mgombea wake Lazaro Ndegea kushindwa kurejesha fomu.

"Bwana mwandishi, napenda kukujulisha kuwa nimejitoa, hivyo sitarejesha fomu na hivi tunavyozungumza muda umeshapita wa kurudisha fomu hizo", alisema  Ndegea akiiambia kwa simu Blogu hii ya jamii.

Akithibitisha  Ndegea kuchemsha Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Igunga Magayane Protace alisema  ni kweli hadi saa tisa na nusu  alasiri alasiri muda wa mwisho kurejesha fomu hizo alikuwa hajaonana na Ndegea.     
Alisema vyama ambavyo wagombea wake wamerejesha fomu na majina ya wagombea hao yakiwa kwenyemabano ni CCM (Dk. Dalaly Peter Kafumu), CUF (Leopard Mahona), CHADEMA (Joseph Kashine), CHAUSTA (Hassan Lutengama), UPDP (Hemed Ramadhani), AFP (Steven Nushuyi),  DP (Saidi Cheni) na SAU (John Maguma).

Protace alisema, tayari majina na sifa za wagombea wa vyama hivyo yamebandikwa kwenye mbao za matangazo kwenye Ofisi za Halmashauri hiyo, na hayakuwa hapo tangu jana saa 10 jioni hadi kesho katika muda huo.

Alosema majina hayo yamebandikwa kwa mujibu wa sheria ili kama kuna mtu au chama kitakachoona kwamba kuna mgombea kwenye kasoro za kisheria kugombea aweke pingangamizi kabla ya saa 24 kuanzia jana saa kumi jioni.

Uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Oktoba 2,mwaka huu, unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Rostam Azizi kujiuzulu wadhifa huo kutokana na sababu za kisiasa.

Wakati kampeni zinaanza rasmi leo, Chama cha Mapinduzi kinazindua kampeni zake Jumamosi kwenye viwanja Samora mjini hapa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages