Breaking News

Your Ad Spot

Oct 15, 2011

NANGOLE: MWANANCHI LIMENILISHA MANENO

NA MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Ole Nangole, amekanusha vikali kumshambulia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye na kusema kwamba gazeti la Mwananchi  limemlisha maneno  kwa manufaa ya kundi la watu wasioitakia mema CCM.

Katika Gazeti la Mwananchi la jana, katika ukurasa wake wa kwanza limeandika  habari yenye kichwa " Mpasuko ndani ya CCM sasa dhahiri' na kumkariri Mwenyekiti  huyo wa CCM mkoa wa Arusha  akimwita Nape kuwa 'muasi namba moja'.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na Uhuru FM (Leo kwa njia ya simu kutoka mkoani Arusha Nangole alisema, Mwananchi limemlisha maneno na karibu habari yote ni uzushi mtupu.

"Hili gazeti la mwananchi wamesema uongo. Habari ya Katibu Mwenezi niliyosema na ambayo nakala yake ipo siyo hIyo, nilizungumzia mkutano wa Umoja wa Vijana hapa Arusha nikasema walikuwa wamefanya vizuri kutaka kuandamana lakini wangefuata taratibu", alisema Nangole.

" waandishi waliponiuliza kuhusu Nape kuhusiana na Vijana hao, nilisema sijui lakini nadhani angewapongeza kwa kuwa wapo katika idara yake, lakini hakuna nilipotamka kabisa kwamba Nape ndiye muasi namba moja" aliongeza.

Akizungumza Nangole alisema, habari hiyo haina msingi wowote wa ukweli badala yake inadhihirisha baadhi ya vyombo vya habari vinavyotumiwa na wapinzani wakiwemo mafisadi ambao wanajaribu kufanya kila linalowezekana uwepo mpasuko ndani ya CCM na hivyo wapate upenyo.

"Hili linaonekana wazi kwamba gazeti hili limetumwa kufanya kazi ya kutuchonganisha ndani ya CCM, na ndiyo sababu baada ya kutafuta maneno ya kunilisha, wakamuuliza Nape kwamba naye anasemaje kuhusu kauli hiyo wakati wakijua wazi kuwa sikusema", alisena Mangole.
Nangole alisema, badala ya kuandika kwa kina habari aliyofafanua kuhusu sakata la kuzuiwa kwa mkutano huo wa Umoja wa Vijana, Mwananchi wamejikita katika kujaribu kuonyesha kuwa amemzungumzia zaidi Nape.
"Kwa mfano katika habari hiyo Mwananchi wameandika kwamba katika mkutano wangu  na waandishi wa habari  nimemtaka Nape aachane na malumbano yasiyo na tija ndani ya Chama na badalka yake asisitize utekelezaji wa Ilani ya CCM na kwamba malumbano hayo yanaashiria dalili mbaya za anguko la Chama hico siku zijazo" alisema Nangole.

Alisema, habari hiyo imeenda mbali zaidi na kudai Nangole amemtaka Nape ajikite kutangaza mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na Chama badala ya kuendeleza malumbano kila kukicha.

" Nimeisoma habari yote kwa kweli imepotosha sana umma, eti wameandika kwamba wakati najibu swali  la mwandishi aliyetaka kujua kauli ya Nape kuhusu kuwepo uasi ndani ya Chama eti nimejibu kwamba ikiwa ni kweli, basi uasi wa kwanza ulifanywa na Nape, kwani aliwahi kutajwa kuwa mwanzilishi wa CCJ, nabari ambayo sikusema kabisa", alilalamika Nangole.

Nagole amesisitiza kuwa mjadala wa kujivua gamba haujaanzishwa na mtu binafsi bali ni maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo katika kufanya mageuzi yake CCM iliona umuhimu wa wote wanaotuhumiwa na kutajwa tajwa na umma kuhusika na vitendo vya ufisadi wapime na kujiengua wenyewe katika vikao vya maamuzi vya chama.

"Katika uamuzi wa kujivua gamba mimi nikiwa mjumbe wa NEC, nilikuwepo ikakubalika kwamba wale wote wanaotajwa tajwa kwa tuhuma mbalimbali katika umma wajiengue wenyewe sasa malumbano yaliyopo sasa ni ya nini?" aliuliza Nangole.

Alisema alichowaambia waandishi wa habari kuhusu kujivua gamba alitaka hatua zifanyike mapema ili kuacha nafasi ya mambo mengine kufanyika. 

Alisema kimsingi alichozungumza alipongeza ziara ya Umoja wa Vijana wa CCM licha ya kuwa chimbuko la malumbano yaliyotokea Arusha na kwamba pamoja na kupongeza lakini alisisitiza kwamba ulipaswa kufuatwa utaratibu katika kufanya mikutano.

"Niliipongeza ziara hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Beno Malisa kwa sababu kimsingi ilikuwa na lengo la kujenga uhai wa Chama wilayani Arusha, lakini kilichokiukwa ni taratibu", alisema.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages