Breaking News

Your Ad Spot

Oct 13, 2011

AIRWING KUENDELEA KUELIMISHA VIJANA KUJITEGEMEA

SHULE ya sekondari ya Airwing imesema itaendelea kutoa elimu  itakayowawezesha vijana kujitegemea ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K.Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari leo shuleni hapo, Mkuu wa shule hiyo, Luteni Kanali Alexius Ndeki, alisema miongoni mwa mambo ambayo Mwalimu aliyapigania ni elimu ya kujitegemea ambayo inawezesha vijana kuendesha maisha yao hata kama wasipopata elimu ya juu ya sekondari.

“Kesho (leo) ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, hivyo na sisi kama taasisi ya elimu tunaungana na Watanzania wenzetu kumuenzi baba wa Taifa, kwetu sisi ni faraja kuona tunayaendeleza yale aliyopenda kwa vitendo,” alisema.

Alisema Baba wa Taifa alipenda kuona Watanzania  wanapata elimu ya kujitegemea, na kwamba shule yake imelienzi hilo kwa kuanzisha chuo cha ufundi katika fani mbalimbali kama ushonaji, udarizi, umeme wa magari na wa majumbani, udereva na ufundi Makenika.

Alisema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha vijana wanaoshindwa kuendelea masomo ya sekondari katika ngazi mbalimbali kupata utaalamu utakaowawezesha kujitegemea baadaye.

“Na hilo ndilo lilikuwa wazo la Mwalimu aliyeamini katika elimu ya kujitegemea” alisema.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages