Breaking News

Your Ad Spot

Nov 6, 2011

AIRTEL TANZANIA NA LEAF TOBACCO ZAPANDA MITI TANGA UZINDUZI WA MICHEZO YA SHIMIWI

Upandaji miti ukifanyika
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya Tobaco TLT mwishoni mwa wiki imejumuika na mamia ya wananchi waliohudhuria michezo ya SHIMIWI inayofanyika katika mkoa wa Tanga  kupanda miti katika shule za sekondari za Galanosi na Ufundi.
Upandaji miti huo umefanywa katika uzinduzi wa michezo hii inayaofanyika mkoani Tanga kwa muda wa wiki mbili kwa kupanda miti elfu tatu.
Halfa hii imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwamo Mgeni Ramsi mkuu wa mkoa wa Tanga Kanali Mstaafu Chiku Galawa pamoja na mkuu wa wilaya ya Tanga Ibrahim Hassan Hussein ambapo nao walishiriki katika upandaji wa miti hiyo.
Wakizungumza kwa katika shughuli hii ya upandaji miti, Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni Kanali mstaafu Chiku Galawa aliwashukuru kampuni ya Airtel na TLT kwa kupanda miti mkoani Tanga na kuwashukuru waandaaji wa michezo ya SHIMIWI kwa kuleta michezo hiyo mkoani hapo ambapo kwa muda wa wiki mbili shughuli za biashara zitaongezeka na kuinua pato la wakazi mkoani Tanga.
Pia aliwaasa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari hizo kutunza mazingira na kuitunza miti iliyopandwa leo na kuhakikisha inastawi na kukuwa kama inavyotarajiwa.
Afisa mazingira wa Airtel bwana Mkama Manyama alisema “leo tunayo furaha kujumuhika na wenzetu shimiwi pamoja na kampuni ya Tobacco TLT katika zoezi la kupanda miti ambalo linaweka historia ya pekee katika shimiwi mwaka huu wa 2011 hapa mkoani Tanga . Sisi Airtel tunachukua nafasi hii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na kutunza rasilimali asili ambazo zitasaidia hadi kizazi kijacho. 
Kwa upande wake mwakilishi wa TLT bwana Fridoline Takisi aliongeza kwa kusema Tanzania Leaf Tobacco imekuwa mstari wa mbele katika kupanda miti kwenye mikoa mbalimbali nchini, hadi sasa TLT kwa kushirikiana na wadau wake imepanda jumla ya miti zaidi ya 10,000 katika miji na mikoa mbalimbali nchini, hii ni katika kutimiza dhima yetu ya kutunza na kuhifadhi mazingira 
Mashindano ya Wizara, idara na mashirika ya umma (SHIMIWI) yameanza rasmi mwishoni mwa wiki hii mkaoni Tanga na yatadumu kwa muda wa wiki mbili mfululizo huku zaidi ya TIMU 42 zikiwa zimethibitisha kushiriki
Katibu wa shirikisho hilo, RAMADHAN SULULU amesema”Sasa Mambo SHIMIWI yameiva, Michezo itakayokuwepo katika mashindano haya ni SOKA, NETIBOLI, MCHEZO WA BAO, KUCHEZA KARATA, Kuvuta kamba na DRAFTI

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages