Naibu waziri wa Fedha Mh Gregory Teu ameutaka uongozi wa chuo cha Mipango na Bodi yake kuangalia uwezekano wa kuwaajiri wahitimu wanaofaulu vizuri masomo yao ili kutumia raslimali zilizoandaliwa chuoni hapo kusaidia wenzao badala ya kusubiri kuajiri kutoka nje.
Ameyazungumza hayo jioni ya leo kwenye mahafali ya 25 ya chuo cha Mipango Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Amesema ni vyema chuo kikaanza kutumia vijana waliofaulu vyema kwenye shahada zao za kwanza kama inavyofanyika kwa vyuo vingine na hatimaye kuwaendeleza kwa ngazi za juu hatua ambayo itasaidia kupunguza pengo la wahadhiri wasaidizi.
Mapema katika taarifa yake mkuu wa chuo hicho Costantine Lifurilo amesema,chuo hicho ambacho kimeanza mwaka 1979 kikiwa na wanafunzi 22, kimeendelea kukua ambapo hadi kufikia mahafali ya leo kimehitimisha wanafunzi 1477 kiwango ambacho amesema kimesaidia kupunguza pengo la wataalamu wa mipango katika ngazi mbalimbali za serikali na hasa serikali za mitaa.
Amesema pamoja na hatua hizo, chuo kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundombinu ya kufundishia na kuiomba wizara kuangalia uwezekano wa kuwezesha ukamilishaji wa jengo la ghorofa saba ambalo litatumika kwaajili ya mihadhara, ofisi na kumbi za kusomea.
Mapema katika salam zake Mwenyekiti wa bodi ya chuo Dr Razack Lokina amesema kwa sehemu kubwa chuo kimeweza kutekeleza malengo yake ya mpango mkakati unaoishia 2014 na kwamba hatua inayokusudiwa sasa ni kuanzisha shahada mbili za uzamili baada ya kukamilisha kwa miundombinu muhimu ya uendeshaji mafunzo hayo.
Amesema hayo yote yamefikiwa kutokana na ushirikiano baina ya chuo hicho, wizara ya fedha ambamo chuo hicho ni sehemu yake, na baadhi ya wadau wahisani kutoka nje.
N
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269