PRESSLEREASE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
MKOA WA SINGIDAWENYEJI MISS UTALII KANDA YA KATI
Master Pub wenyeji Miss Utalii Vyuo Vikuu Dodoma-Talent
Habari za muda huu ndugu zangu wote, napenda kuwakaribisha katika Mkutano huu wa kuwatambulisha mkoa ambao utakuwa wenyeji wa mashindano ya Kanda ya kati unaoshirikisha mikoa ya Dodoma,Singida,Tabora na Katavi.
Wasomi wengi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini wameendelea kujitokeza katika Mashindano ya Miss Utalii Tanzaniayanayoendelea kufanyika katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Tabora,Singida,na Katavi ambao Fainal zake zinaendelea katika maandalizi huku kukiwa na ushindani mkali kutokana na washiriki wengi kuwa wasomi wa Vyuo Vikuu na wanafunzi wa Elimu za ngazi za juu.
Mkoa wa Dodoma ndiyo pekee ambao Tayari umeshamaliza Fainali zake huku Tayari warembo wakiwa wameshapatikana kwa ajili ya kushiriki ngazi ya Kanda itakayofanyika kwenye mkoa wa Singida mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili.
Tabora ambao wako kwenye maandalizi Fainali zake zimepamgwa kufanyika tarehe 25 mwezi wa 12, Singida wenyewe Fainali zimepamgwa kufanyika tarehe 3 mwezi wa 12 na Katavi fainali zikiwa zimepangwa kufanyika tarehe 30 ya mwezi wa kumi na mbili, Vyuo Vikuu Dodoma Fainali zake zitafanyika Tarehe 18/11/2011 kwenye ukumbi wa Royal Village lakini kabla yake kutafanyika fainali ya kupata mshindi wa Vipaji kwenye Klabu mpya na ya Kisasa ya Master Pub tarehe 15/11/2011.
Baada ya kukamilisha fainali hizo idadi ya warembo 24 watakaoingia hatua ya kanda ya kati fainali zake zitafanyika katika mkoa wa Singida ambapo tarehe itapangwa baada ya kamati ya Kanda kukutana na kasha kuamua siku na Tarehe ya mashindano.
“Maandalizi yanakwenda vizuri, na ni jambo la kujivunia kuona vijana wetu wanajitokeza kwa wingi kujiunga na mashindano haya kwenye ngazi za Mikoa .
Tunawashukuru wadhamini mbalimbali wanaojitokeza kudhamini na kuunga mkono juhudi za Miss Utalii Tanzania za kutangaza vivutio vyetu vya utalii,utamaduni na mianya ya uwekezaji ya Tanzania.
Tunawashukuru zaidi wenzetu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuweza kujitokeza katika kuunga juhudi za kufanikisha fainali zilizomalizika juzi ambapo Grece Saimon aliweza kuibuka mshindi baada ya kuwashinda wenzake 14 waliokuwa kwenye maandalizi.
Tunafarijika zaidi pale tunapoona kampuni za kizalendo na wazalendo wanajitokeza zaidi kudhamini shindano hili,na hata wajasiliamali ambao wanajitokeza kutudhamini.Tunaamini hii ni kutokana na ukweli kwamba shindano la Miss UtaliiTanzania linaendeshwa na wajasiliamali wazalendo,kwa manufaa ya taifa na watanzania wote,tena kwa kuzingatia mila ,desturi na utamaduni wa mtanzania.
Kampuni ya Peter Fashion pamoja na kampuni zake tanzu za Peter Palm Hotel, Peico, walidhamini shindano hili,kwa thamani ya jumla ya shilingi milioni mbili zilizo husisha pesa taslim na huduma kwa ajili ya zawadi,usafiri na huduma nyinginezo ikiwemo maandalizi ya washindi kwa ajili ya kushiriki fainali za kanda ya kati.
Mkurugenzi wa Peter Palm Hotel, Emmanuel Peter ametaja baadhi ya sababu za kudhamini shindano hili kuwa ni pamoja na kuvutiwa na mfumo mzima wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania,ikiwemo wa kuwafundisha washiriki kucheza na kuimba nyimbo na ngoma za asili za makabila mbalimbali ya Tanzania jambo ambalo ni adimu katika mashindano mengine kuonekana.
“kwa muda mrefu tumekuwa tukifuatilia mashindano haya ambayo kwa hakika yamekuwa mstari wa mbele kuutangangaza utalii na utamaduni wetu kitaifa na kimataifa na hata kuwa ndilo shindano linalofanya vizuri zaidi kimataifa. Lakini tunaona kuna tatizo kwa wadhamini kuto kudhamini shindano hili kwa visingizio mbalimbali,sisitunaamini kuwa ni kutokana na ukweli kwamba wamiliki wa makampuni mengi makubwa si watanzania ambao hawaoni uthamani wa utamaduni wetu wala haja ya kuutangaza,ndiyo maana wanadhamini mengine ambayo hayana manufaa kwa taifa wala Tanzania.Tunatoa wito kwa makampuni mengine ya kizalendo yajitokeze kudhamini shindano hili la kizalenda,kijasiliamali na kielelezo halisi cha utanzania na utamaduni wetu,alisema Emma.
Wadhamini wengine waliojitokeza kusaidia ni Mlonge By Makai Enterprisess, Kitoli Hill Hoteli, Ngoto Feniture, Laazizi Klabu, Perugina Investment Campany limited, shaabanmpalule.blogspot.com,New Dodoma Hoteli, Haji Mapoda Cosmetic, Master Pub, City Boys, Tanzania Daima & Sayari News Paper, Mwangaza FM Radio, Clouds Fm, Dar City College, Asaah Saloon, Salama Saloon, na Chicnos Investment,
Mikoa ambayo Tayari imeshamaliza fainali zake za Miss Utalii 2011/2012 ni Mbeya, Mara, pamoja na Dodoma,
Asante,
CONRAD MAPUNDA
MKURUGENZI MISS UTALII VYUO VIKUU KANDA YA KATI
Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage - Do Value Added Pageant"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining"
Regard,
Gideon E.G. Chipungahelo
PRESIDENT / C.E.O
Hotline: + 255 - 715/754/773 - 318 278.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269