Rais Jakaya Kikwete amewataka wadau wa elimu kushirikiana katika kubaini vitabu vya kiada vilivyojaribiwa, tahiniwa na kupimwa (tried and tested text books) kwa ubora wake kama moja ya njia muhimu za kuinua kiwango cha elimu nchini.
Amesema kuwa walimu wa Tanzania wakipatiwa vitabu hivyo wanao uwezo wa kufundisha somo la Kiingereza vizuri.
Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Novemba 14, 2011, Ikulu, Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bibi Katy Allen, mtunzi wa vitabu vya lugha ya Kiingereza vya Oxford.
Bibi Katy Allen alikuwa anamwelezea Rais Kikwete kuhusu jitihada ambazo shirika lake lisilokuwa la kiserikali la Village Education Project Kilimanjaro (VEPK) limekuwa linafanya kuchapisha na kuboresha kutunga vitabu vya kufundishia na kujifunza lugha ya Kiingereza vya Oxford Engilish Books vilivyokuwa vinatumika kufundishia lugha hiyo nchini katika miaka ya nyuma.
Bibi Katy Allen anasema kuwa shirika lake linaamini kuwa kama vitabu hivyo vikianza kutumika tena katika shule za Tanzania, ufundishaji wa lugha ya Kiingereza unaweza kuboreka haraka zaidi.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete amesema kuwa ni dhahiri walimu wa Tanzania wanaweza kufanya kazi nzuri zaidi kama watawezeshwa na wadau mbalimbali wa elimu kwa njia nyingi ikiwa ni pamoja na kupatiwa vitabu bora zaidi vya kiada vya kuongoza namna bora zaidi ya mbinu za ufundishaji.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwelezea kiongozi huyo kuhusu fursa za uwekezaji zilizoko Tanzania hasa katika eneo la nishati na madini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269