Breaking News

Your Ad Spot

Nov 21, 2011

TANZANIA KUKUBALI KUWA NA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA WAHALIFU WA KIVITA NA MAUAJI YA KIMBALI

Serikali imetaja mambo makuu matano yatakayoifanya Tanzania kukubali kuanzishwa kwa Mahakama ya ICC na kusema pamoja na mambo mengine Mahakama hiyo itakuwa na uwezo wa kusikiliza na kutoa hukumu kwa watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya mauaji ya kimbali na ya Kivita hata kama watuhumiwa watakuwa wametoka nchi nyingine.

Mambo hayo yametajwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohammed Chande Othman, wakati akifungua mkutano uliojadili masuala mbalimbali ya kisheria unaofanyika mjini Zanzibar mkutano ambao pia unajadili Mkataba wa Roma unaozitaka nchi mbalimbali kuanzisha Mahakama ya ICC.

Miongoni mwa mambo yanayopelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo ni kuwa na uwezo kisheria ya kuanisha taratibu za kukamatwa na kushitakiwa na kutoa hukumu ama kuwakabidhi watuhumiwa kwa nchi nyingine watuhumiwa wanaokabiliwa na makosa kama hayo.

Mh. Chande amesema kuwa kwa vile Mahakama hiyo itakuwa tofauti na mahakama nyingine kwa vile mahakama hiyo haitakuwa na Askari Polisi na badali yake itategemea uwezo wa kisheria na mashirikiano na mataifa mengine katika kuwakabili watu waliokimbia kutoka nchi moja kwenda nyingine hali wakikabiliwa na tuhumiwa za kutenda makosa hayo katika nchi walikotka.

Hata hivyo pia Jaji Mkuu ametoa wito kwa wabunge na Wajumbe wa baraza la Wawakilishi kuwa utakapofika mbele yao mswada huo, waujadili na kuupitisha kutumika kama sheria kwa kuupa nguvu ya kisheria ili kuupa uwezo wa kutekeleza majukumu yake kama sheria.

Lakini pia kwa kupitishwa kwa mswada huo, kutaiwezesha Tanzania kushirikiana na ICC katika mambo mbalimbali ya kisheria na kusaidia kudumisha ushirikiano wetu na mataifa mengine katika utekelezaji wa majukumu yake.

Naye Mkurugenzi wa Wanasheria kutoka Tume ya Kimataifa ya Wanasheria tawi la Kenya Bw. Jack Muriuki, akizungumza katika mkutano huo, amesema kuwa kama mahakama hiyo ingekuwepo nchini Kenya tangu miaka ya nyuma, ingeweza kushughulikia kesi za vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi Mkuu uliopita.

Amesema kuwa tayari hivi sasa Kenye imeridhia kuanzishwa kwa Mahakama hiyo na kwamba itakapokuwa tayari, inaweza kushughulikia kezi zote za mauaji ya wenyewe kwa wenyewe ama ya kijeshi isivyo halali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Children Education Society (CHESO) Bw. Richard Shilamba, ambaye pia ni Mratibu wa mkutano huo, amesema kuwa mkutano huo ni sehemu ya kimafunzo kwa wanasheria, wabunge pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili kusaidia kutoa msukumo na kujenga uwelewa juu ya utendaji wa mahakama hiyo.

Amesema kuwa Mahakama hiyo itakuwa na uwezo wa Kisheria kumshughulikia kisheria mtu yeyote yule atakayetenda makosa hayo yaliyotajwa bila kujali itikadi ama uzito wa madaraka yake.



Wengine wanaohudhuria mkuno huo, ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omari Othman Makungu, Wataalam wa Sheria kutoka baadhi ya nchi za Ukanda wa Afrika ya Mashariki pamoja na Wanahabari.                 

 Source: 0788 6488 / 0715 886488 / 0767 886488

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages