Breaking News

Your Ad Spot

Nov 21, 2011

KAMATI KUU YA CCM YATEUA MAKATIBU WAPYA KUMI WA CCM

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo
katika siku ya kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea
mjini Dodoma imefanya uteuzi wa makatibu 10 wa CCM wa wilaya .
Makatibu wa wilaya wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo: -

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye imewataja wapya walioteuliwa kuwa ni:-

1. Ndg. Zainabu Mlawa,
 2. Ndg. Paulo Mwita,
3. Ndg. Magdalena Ndwete,
 4. Ndg. Ramadhani Sevingi,
 5. Ndg. Odilia Maholelo,
6. Ndg. Omari Zuberi Mbwana
7. Ndg. Raymond Mangwala,
 8. Ndg. Yahya Saleh Issa,
 9. Ndg. Ame Omar Mkadam
10. Ndg. Langael Akyoo

Pia Kamati Kuu ya CCM imetengua uteuzi wa Makatibu watatu wa wilaya
na kuwapangia kazi nyingine. Makatibu hao ni:-
1. Ndg. Zubeda Mbarouk aliyekuwa Kwimba
2. Ndg. Mussa Wenema aliyekuwa Kilindi
3. Ndg. Mkongea Ally Pira aliyekuwa Wilaya ya Magharibi.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa inafanyika tarehe 21 na
22/11/2011 na kufuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa
kitakachofanyika tarehe 23 na 24/11/2011.

Kikao hicho na vingine vinafanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Baada ya kumalizika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 25 hadi 27/11/2011 kutafanyika Semina ya Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi wa
ngazi ya Kitaifa hadi Wilaya.

Katika semina hiyo watakaoshiriki ni Wajumbe wa Sekretarieti ya
Halmashauri Kuu ya Taifa, Sekretarieti za Jumuiya za Chama Cha
Mapinduzi (UWT, UVCCM na WAZAZI), Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya
zote nchini.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Benjamin Mkapa, Mjumbe wa Kamati Kuu, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abein Karume na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Kushoto ni wajumbe wa Kamti Kuu ya CCM.

1 comment:

  1. Hivi siku hizi CCM ni chama cha kidini? Zamani walau kulikuwa na uwiano sawa...angalia sasa idadi kubwa ni dini moja naona mwenyekiti ameamua anataka kuacha historia...

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages