Breaking News

Your Ad Spot

Nov 21, 2011

MACHAFUKO YA KISIASA MALAWI YATIBUA MICHUANO YA 'POLL ALL AFRICA CUP 20011'

Mashindano ya mchezo wa pool ya ALL AFRICA CUP 2011 yaliyokuwa yafanyike  kuanzia kesho, Novemba 22 hadi 26, mwaka huu,  Blantyre, Malawi, yameahirishwa kutokana na  machafuko ya kisiasa nchini humo.
Kufuatia mashindano hayo kuahirishwa, safari ya  timu ya Taifa ya Poll ya Tanzania iliyokuwa imeanza wiki iliyopita imeota mbawa.

Akitangaza  kuahirishwa kwa safari ya timu hiyo,  Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema  sasa Bia ya Safari  imeandaa ziara ya timu ya Taifa ya Pool katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, baada ya kushauriana na chama cha mchezo huo ili kuwafanya wachezaji wa timu ya taifa kuwa katika hali ya mchezo na kufanya mazoezi baada ya kuahirishwa kwa mashindano hayo.

Akizungumzia na mtandao huu kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu ya 'ALL AFRICA CUP –MALAWI' yamefutwa kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wa chama cha pool Africa lakini tumefarijika sana kuona kwamba Bia ya Safari Lager bado iko na sisi bega kwa bega na kuipa nafasi timu yetu kufanya ziara ya michezo ya kirafiki na timu za mikoa’’ alisema katibu.

Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho, Isaac Togocho alisema “ Tulipokea taarifa za kufutwa mashindano kwa masigitiko makubwa sana kwani tulikuwa tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo, lakini nilifarijika sana kusikia kuwa wadhamini wetu SAFARI LAGER wametupa nafasi ya kujiandaa zaidi kwa kutupa michezo ya kirafiki katika mikoa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages