Idadi ya waliokufa katika ajali ya basi la Taqwa lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Burundi lililogongana uso kwa uso na roli Wilayani Biharamulo mkoani Kagera imeongezeka na kufikia 18.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Henry Salewi alisema kuwa ajali hiyo iliyotokea katika barabara ya Rusahunga /Nyakahura iliyoko Wilayani humo, Novemba 19 mwaka huu, saa 4.30 asubuhi ilisababisha fifo vya watu 11 kufa papo hapo na kujeruhi wengine 24.
Kamanda Salewi alisema idadi hiyo imeongezeka kwa watu saba wengine kufa wakati wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo na kuwataja marehemu ambao miili yao imechukuliwa na ndugu na jamaa zao kwa ajili ya mazishi kuwa ni Elick Eliud (18) mkazi wa Ngara ,Aziza Saidi (60) wa Tabora na Ali Issa (35) wa Dar es Salaam.
Aliwataja wengine waliotambuliwa na ndugu zao kuwa ni Farda Abdallah (35)mkazi wa Tabora,Chinuka Amajatha (30-35) mwanafunziwa chuo kikuu cha Dar es salaam raia wa zambia,dreva wa basi hilo Sultan Mohamed (36) mwenyeji wa Kahama ,Dreva wa roli,Luzindana Theonest (35) Mnyarwanda na Abiba Juma (45) mkazi wa Tabora ambapo kati ya hao waliotambuliwa kuna marehemu watatu wa familia moja ambapo kamanda hakuweze kuwataja majina.
Kamanda alisema kuwa majeruhi mpaka sasa ni 17, huku waliolazwa katika Hospitali teule ya Ngara Omulugwanza kuwa ni watano na kumi na wawili wakiwa wamelazwa katika hospitali teule ya Biharamulo kati yao watano hari zao ni mbaya maana hawajajitambua mpaka hivi sasa.
Aliyataja majina ya majeruhi waliojitambua na kutambuliwa na ndugu zao kuwa ni Joseph Bartazal (24) mkazi wa Ngara,Said Suleiman(4)mkazi wa Tabora,Ntaband Ansert (29) Raia wa Burundi,donard Richaa (20) mkazi wa Ngara,Joseph Bugirimana (34) mkazi wa Dar es Salaam ila ni raia wa Burundi,Pina Elisha (12) mkazi wa Ngara na Jane Kasanga (46) mkazi wa Dar es Salaam waliolazwa katika hospitalia ya Wilaya ya Biharamulo na hari zao zinaendelea vizuri.
Aliwataja majeruhi wengine waliolazwa katika hopsitali ya Omulugwanza iliyoko Wilayani Ngara kuwa ni Agineta Sewita (53) mkazi wa Ngara,Andongwise Mwakisisile (39) mwalimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam,Samweli Lusulo (46) mkazi wa Ngara,Arbert Dafula umri wake hahujajulikana ni fundi seremala mkazi wa Dar es Salaam na Kabula Ismail (27) mkazi wa Bujumbura.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa madreva wa magari yaliyohusika na ajali hiyo ambao nao wamekufa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269