Breaking News

Your Ad Spot

Nov 20, 2011

MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE KUSIMAMIA VIKAO VYA CCM DODOMA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa na vikao vyake vya kawaida vitakavyofanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 21 – 27 Novemba, 2011, vyote vikiwa chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye imesema Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa itafanyika tarehe 21 na 22/11/2011 na kufuatiwa na kikao cha siku mbili Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika tarehe 23 24/11/2011.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo  kwa vyombo vya habari ambayo imesainiwa na Nape, baada ya kumalizika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 25 hadi 27/11/2011 itafanyika Semina ya Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi wa ngazi ya Kitaifa hadi Wilaya.

"Katika semina hiyo watakaoshiriki ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Sekretarieti za Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (UWT, UVCCM na WAZAZI), Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya zote nchini", ilisema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages