Breaking News

Your Ad Spot

Nov 18, 2011

UKOO WA CHADEMA BUNGENI WAANIKWA: UHURU

BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.
 
"Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa Mwenyekiti wa Chama ana ndugu watatu, Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme? Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, Samahani Mh. Ndesamburo"

Akichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011,
Assumpter Mshama (Nkenge –CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.

“Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi,” alihoji.

Aliongeza: “Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.

“CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje.”

Kwa upande wake, Livingstone Lusinde
(Mtera-CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.

Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku.

“Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme,” alisema.

Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo kwani wa kuzuia fujo wapo.

“Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu,” alisema.

Lusinde aliohoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.

Mbunge huyo alisema CHADEMA inafanya hivyo kutokana na ahadi ya fedha waliyopewa na Ujerumani.

CHADEMA imesusa kujadili muswada huo unaohitimishwa leo, baada ya kujadiliwa kwa siku nne, kwa kile wanachodai umekosa uhalali kwa kukiuka Kanuni za Bunge.

Hata hivyo, CHADEMA imekuwa ikijibu hoja zinazojadiliwa na wabunge bungeni, kupitia mikutano na waandishi wa habari inayofanyika kila siku mchana, ambapo katika mkutano wa jana imeliomba bunge kutopitisha muswada huo.

Mikutano hiyo imekuwa ikiitishwa na viongozi wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo) na Tundu Lissu (Singida Mashariki), ambaye Jumatatu wiki hii aliwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, kuhusu muswada huo.

Katika maoni hayo, alipendekeza baadhi ya mambo kwenye muswada huo na pia aliwachefua wabunge kutokana na hoja zake kuhusu Muungano na pia kutamka kuwa Tanzania ina urais wa kifalme.

John Lwanji (Manyoni Magharibi-CCM), alisema wanachofanya CHADEMA ni sawa na kiini macho katika mazingaombwe, akitumia neno abrakadebra.

Benardetha Mushashu (Viti Maalumu-CCM), alihoji CHADEMA walitoka bungeni kwa kanuni gani na mbona hawachukuliwi hatua.

“Wanawalaghai wananchi, Lissu alichangia muswada. Wanaharakati wanatangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kama kwamba hakuna serikali, wakijaribu wataona,” alisema.

Alisema kinachoendelea Arusha ni matokeo ya maandamano ya kila siku, ambayo hivi sasa yameanza kushamiri Mwanza, ambapo watu wanapigwa mabomu ya machozi.

“Libya walianza na maandamano, Gaddafi ameuawa, lakini hivi sasa wanauana,” alisema.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hamlazimishi mbunge kuingia kwenye kamati, bali anachofanya ni kufuata Kanuni za Bunge na Katiba.

Alisema hayo bungeni jana, kutokana na malalamiko yanayotolewa na CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwamba, spika alilazimisha wabunge kuingia katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kujadili muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.

Spika Anne alisema CHADEMA hawakutumia busara kutoka ndani ya ukumbi wa bunge, bali wangewasilisha hoja zao, na endapo wangeshindwa, basi wangeshindwa kishujaa.





6 comments:

  1. kaka acha propaganda hizo, kina January Makamba siwameingia kwenye siasa sababu ya baba yake, huyo rafiki yako unayempamba kwenye blog yako Nape si sababu ya jina la baba yake, alikuja hapa DMV alidhani tutaenda kumsikiliza yeye ni nani? New York walimwambia ukitaka kukutana na Watanzania kutana na Wana CCM na siyo watanzania...sisi tunakutana na viongozi wa serekali siyo chama bwana.

    Chadema walichofanya ni sahihi kabisa, huo mchakato wa katiba kuna haraka gani...lazima wananchi washirikishwe...kaka Watanzania wa sasa ni wasomi watapigania haki zao mpaka kieleweke...hawakwenda kusoma certificate ya Uhandishi wa habari wengi wao sasa wapo kwenye Elimu za Juu...sasa badala ya kujadili mambo muhimu wanaongelea Chadema...

    ReplyDelete
  2. we pumbavu tena najuta hata kuingia kwe hii blog

    ReplyDelete
  3. Kaka hii si propaganda. Nimeichapisha ili iweze kuonwa na wengi. Wapo watakaoona ni sahihi na watakaoona tofauti! Hiyo ndiyo raha ya Uhuru wa kutoa mawazo!

    Kaka hilo la Januri na Nape ningefurahi zaidi kama watajibu wenyewe. Lakini nachoamini ni kwamba hawakubebwa na baba zao, isipokuwa wametokea kuwa wana siasa kwa sababu za kawaida kama vile mtoto wa mkulima anapokuwa si ajabu kuwa mkulima, wa mvuvi kuwa mvuvi na wa mwanasoka kuwa manasoka

    Lakini taja ni Kiongozi gani wa ngazi ya Juu wa CCM ambaye yeye na mkewe, mkwewe, mjukuu wake, mpwawe au shangazi yake ambao wote kwa pamoja ni wabunge katika bunge la sasa!

    Inawezekana CHADEMA wamefanya sahihi kuchukuana. Lakini itakuwa sahihi zaidi kama wamefanya hivyo kama Chama hicho hakina watu wakutosha wenye uwezo, kinaowaamini kuweza kuwa wabunge viti maalum.

    Vinginevyo kaka Mti hujulikana kwa matunda yake! Tunapotaka kujua udhati wa hoja inayotoka mdomoni kwa mtu tunamtazama yeye kwanza. Siyo "Fuata neno langu usifiate matendo yangu!"

    Kweli mchakato wa Katiba hauna haraka, ingawa ninashangaaa kwamba wale wale wanaoona hauna haraka ndiyo mwanzoni kabisa walisema "tunataka katiba haraka" tena kwa maandamano!

    KARIBU!

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo juu umenena, Nape alipokuwa hapa DC alitaka kukutana na wabongo...yeye anadhani sisi ni watu wa vyama...muda huo hatuna.

    ReplyDelete
  5. Tatizo la nchi yetu kwa sasa ina wasomi wengi ambao hawajaelimika na wakulaumiwa ni serikali hii iliyopo madarakani.
    Blogger alichofanya ni kutuletea habari kutoka bungeni na kufafanua zaidi yale yaliyosemwa na wabunge inashangaza kuona watu wanaanza kumshambulia yeye binafsi.
    Tungeonekana tumeelimika kama tungeishambulia habari yenyewe na siyo mleta habari.
    Wengine tunadiriki kumtukana mleta habari, hii siyo busara ya mtu aliyeelimika bali ni busara ya mtu ambaye hajaelimika. jamani tujalibu kujielimisha angalau wenyewe pamoja na kwamba serikali hii haikutupatia fursa ya kufanya hivyo ili tuwe na uwezo wa kujenga hoja na siyo kuwa na hoja za nguzu zinazoambatana na munkari.
    Mawazo kama haya yanachochea udikteta wa fikra katika jamii na hii ni kichocheo cha kudumaa.
    Jamani elimu haina mwisho.

    ReplyDelete
  6. kaka unayejiita msomi unamaanisha nini? inawezekana ndo walewale wa digirii za .com kukopi na kupest kitu kiko wazi uso elewa kipi na usomi wako?huna hoja labda ni walewale wakukaririshwa "Ma brain washed"

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages