CHAPISHO LA PATO LA MKOA WA IRINGA
Utayarishaji wa Pato la Mkoa wa Iringa umekamilika.
Kazi hii imefanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.
Kazi kubwa ilikuwa ni ukusanyaji wa taarifa ya uzalishaji wa bidhaa na huduma katika Mkoa wa Iringa kwa miaka iliyokusudiwa ambayo ni mwaka 2006, 2007 na 2008.
Dhumuni kuu ni kutoa viashiria vya Pato la Mkoa, Pato la Wilaya ya Wastani wa Pato kwa Mkazi ambayo vitatumika katika kutathmini sera mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya umaskini katika Mkoa wa Iringa.
Matokeo haya yatatangazwa rasmi 20 Desemba, 2011 katika mkutano wa wataalamu wa Mkoa wa Iringa (RCC) tarehe 20 Desemba, 2011 mnakaribishwa.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu inahimiza wote kuwa kutoa Pato la Mkoa wa Iringa itakuwa ni chachu kwa Mikoa mingine ambayo haijafanya zoezi hili.
TAKWIMU KWA MAENDELEO
ASANTENI
Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu
S. L. P. 796 Dar es Salaam.
Simu +255 22 2122724, +255 22 2122722/3
Fax: +255 22 2130852
Barua pepe: dg@nbs.go.tz
Tovuti: www.nbs.go.tz
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269