Breaking News

Your Ad Spot

Jan 21, 2012

NAPE ANOGESHA BONANZA LA WAFANYAKAZI WA SAHARA COMMUNICATIONS LTD MWANZAAA

 Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wapili kushoto) akishiriki mchezo wa kuvutana kwa kamba uliofanywa na wafanyakazi wa Sahara Communications Ltd, mjini kwenye ufukwe wa ziwa Victoria jijini Mwanza leo. Upande wa Nape ulishinda.
 Upande wa Nape ukizidisha kasi ya kuwavuta wa upande wa pili ambao walianza kuanguka
 Hatimaye upande wa kushoto wakaibuka washindi wamchezo wa kujifurahisha wa kuvutana kwenye kamba
 Nape na baadhi ya wachezaji wa mchezo wa kuvuta kamba waliokuwa upande wake, wakishangilia baada aya kuwashinda wenzao
 Mchezo kama huo pia ulifanywa na kina dada wa kampuni hiyo kama hivi
 Kutokana na Bonanza hilo kuwa la muhimu ilibidi kamera nyingi zitunmike, Huyu ni Fatuma Shemweta akipiga picha matukio katika bonanza hilo.
 Baada ya kushiriki mchezo wa kuvutana kwa kamba Nape akizungumza  mawili matatu na wafanyakazi wa kampuni hiyo, Pamela na Mary.
 Lakini Bonanza hilo likamkutanisha pia Nape Steven Mhozya (kulia) ambaye walisoma wote shule ya sekondari Nsumba jijini Mwanza miaka yab 90.
 Kina dada wa kampuni hiyo wakifurahia michezo
 Kuleni pozi basi: Fatuma Shemweta aakiwaambia Mariam na Grory wakati akiwapiga picha
 Muhsin Mambo aka MC Stoper nsiye alikuwa MC wa shughuli yote ya bonanza hilo
 Hata baadhi waliweza kwenda na vichanga vyao kwenye bonanza hilo kama huyu dada aliyekuwa akimnywesha uji mtoto wake huku dada mwingine akifurahia picha
Kwa kina dada waliokuwa kwenye bonanza hilo vivazi navyo vilishindana kama hivi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages