Breaking News

Your Ad Spot

Jan 28, 2012

NAPE KUUNGURUMA STAR TV KESHO ASUBUHI, KUHUSU MAADHIMISHO YA MIAKA 35 YA CCM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kesho atakuwa katika studio za Kituo cha Televisheni cha Star Tv jijini Dar es Salaam, kuzungumzia kwa kina sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya  CCM mwaka huu.

Wakati Nape (Pichani) atakuwa katika studio za jijini Dar es Salaam, katika kipindi hicho kitakachorushwa kuanzia saa moja asubuhi (7.00 am), Kada wa CCM Frank Uhahula atakuwa akizungumzia suala hilo hilo akiwa katika studio namba moja za Star Tv zilizopo jijini Mwanza.

Bila shaka hii itakuwa fursa nzuri kwa wale wote wenye dukuduku la kutaka kufahamu kwa kina mambo mengi kuhusiana na maadhimisho hayo ya miaka 35 ya CCM 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Mapema mwezi huu kuhusu maadhimhso hayo, Nape alisema katika sherehe hizo mambo mengi yatajiri.
Nape alisema kwa kuwa maadhimisho hayo yanafanyika wakati uchaguzi mkuu wa chama unakaribia, Chama kitayatumia kupiga vita wagombea wote wanaotoa na kupokea rushwa wakati wa uchaguzi huo.

Chama kitatumia maadhimisho hayo kuhamasisha wananchama wake waadilifu na waaminifu kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika mwaka huu, kuanzia ngazi za mashina hadi taifa.

Nape alisema, pia fursa hiyo itatumika kuelimisha wanachama na wananchi kwa jumla kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi yanayokusudiwa kufanyika, ikiwa ni pamoja na msimamo wa kuilinda nchi, amani, na kupatikana kwa Katiba bora itakayokuwa na manufaa kwa watu wote.

Alisema, maadhimisho hayo yataanza Januari 30, mwaka huu kwa shughuli mbalimbali zilizoratibiwa katika ngazi mbalimbali za Chama mikoani hadi  Taifa,  mpaka Februari 5, 2012 maadhimisho hayo yatakapohitishwa kwa matembezi ya mshikamano yatakayofanyika kila mkoa huku Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo kitaifa mkoani Mwanza.

"Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Mapinduzi kufikisha miaka 35 ya uhai wake yangu vyama vya TANU na ASP vilipovunjwa na kuundwa chama kipya cha CCM chenye nguvu, Februari 5, 1977",lisema Nape na kuongeza.

"Sherehe hizo huadhimishwa kwa Chama na Jumuia zake kufanya shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii. Aidha, Kitaifa Chama huteua mkoa mwenyeji wa sherehe hizi ambazo huambatana na matembezi ya mshikamano".

Alisema kwa kuwa mwaka huu ni wa Uchaguzi Mkuu wa Chama kimependekeza kaulimbiu mahsusi itakayotumika katika sherehe hizo kuwa ni "CCM Imara na Madhubuti inaanza na mimi; naimarisha Chama Changu kwa kuchagua viongozi bora na waadilifu".

Nape alisema uzinduzi wa sherehe hizo utafanyika kila mkoa Januari 30, mwaka huu na kufuatiwa na wiki ya shughuli za Jumuia, ambazo kila Jumuia itapanga ratiba ya mikutano ya ndani na shughuli za kijamii kama kupanda miti, ukaratabti wa shule, zahanati na kadhalika.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages