Breaking News

Your Ad Spot

Jan 23, 2012

SUMARI AZIKWA, AKERI ARUMERU: JK AONGOZA WAOMBOLEZAJI

Rais Kikwete akiweka shada la maua mazishi ya Sumari
RAIS Jakaya Kikwete leo amewaongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya aliyekua mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki(CCM)Jeremiah Sumari.

Sumari alifariki dunia januari 19 mwaka huu jijini Dar es salaam kwa ugonjwa wa saratani ya ubongo.

Katika maziko hayo yaliyofanyika kijiji cha Akeri wilayani Arumeru katika makaburi ya familia ya marehemu Mzee Solomoni Sumari ambapo ndipo alipozikwa pia marehe baba yake huyo, pamoja na Rais maziko hayo pia yalihudhuriwa na waziri mkuu Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Anne Makinda, Naibu spika Job Ndugai, Waziri wa nchi Sera na Bunge Willium Lukuvi, waziri wa nchi ofisi ya Rais mahusiano Steven Wasira.

Wengine ni waziri wa nishati na madini Willium Ngeleja, waziri wa afrika mashariki Samwel Sitta, Naibu waziri wa nishati na madini Adam Malima, naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Godluck Ole Medeye, mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowassa na wabunge mbalimbali.

Akizungumza kabla ya maziko hayo waziri mkuu Pinda alisema serikali ya CCM inaahidi kutimiza ahadi zote zilizotolewa na marehemu Sumari kwa jimbo hilo ndani ya kipindi kifupi tangu kufariki kwake hapo Januari 19.

Alisema Sumari aliahidi ahadi hizo kama mtu binafsi lakini kwakua sasa amefariki jukumu hilo litakua ni la serikali, chama chake cha CCM kwa kushirikiana na halmashauri na wananchi wa jimbo hilo.
 
Aliwataka wanafamilia akiwemo mjane wa marehemu huyo pamoja na watoto wake kutokata tama kutokana na msiba huyo bali waone kama ni changamoto kwao ili kuendeleza yale yote mazuri aliyoyaanzisha marehemu baba yao.

Nae spika wa bunge Anne Makinga alisema bunge limempoteza mbunge muhimu katika ushauri wa masuala mbalimbali ya fedha kwakua alikua akitumika sana katika kutafuta majibu ya mambo yaliyokua magumu katika bunge lake kuhusu fedha.

Alisema mbunge huyo alikua mwadilifu katika kazi yake halia mbayo inapaswa kuigwa na viongozi wengine wa umma katika kujiuliza wao wamejiandaaje mara siku za maisha yao zitakapokamilika.

Katika hali isiyo ya kawaida spika Makinda aliwamwaga machozi waombolezaji pamoja na wanafamilia pale alipoongoza kuimba wimbo wa mapambio uitwao “Nataka Nimwone Yesu” unaodaiwa ulikua ukipendwa zaidi na marehemu Sumari wakati wa uhai wake.

Nae naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kwa niaba ya kiongozi wao Zitto Kabwe akitoa salamu za rambi rambi kufuatia msiba huo alimsifu mbunge huyo aliyewahi kuwa naibu waziri wa kazi ajira na vijana na pia naibu waziri wa fedha katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais Kikwete kwamba alikua mwadilifu na mchapakazi.

Zitto alisema marehemu Sumari alikua mwanasiasa aliyekua na kipaji kwakua alikua akifanya kazi zake kwa ufasaha na hata katika kujibu maswali bungeni alikua akijibu kikamilifu hali iliyowasababisha wao kuuliza tu maswali ya nyongeza wandelee kumsikia akizungumza.

Kufuatia msiba huo kambi hiyo ilitoa ubani wa shilingi 2,350,000 wakati CCM na wabunge wake wakichangia ubani wa shilingi 10,000,000 wakati michango hiyo ikiwa ni tofauti na ile ya serikali ambayo kwapamoja inakamilisha kiasi cha zaidi ya shilingi 20,000,000.

Kifo hicho kinafikisha idadi ya wabunge wawili waliofariki katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja akimfutia mbunge wa viti maalumu Chadema Regia Mtema aliyefariki dunia kwa ajali ya gari mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages