Breaking News

Your Ad Spot

Jan 13, 2012

TUSKER YA KENYA YAWASILI DAR KUIKABILI SIMBA

TIMU ya soka ya Tusker ya Kenya imewasili jijini Dar es Salaam leo tayari kwa pambano lake la keshokutwa (Jumapili)  dhidi ya Simba SC litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini.
Tusker imewasili ikiwa na kikosi kamili cha wachezaj 20 na viongozi watano tayari kwa pambano hilo linalotarajiwa kuwa kali na la kusisimua.

Tusker sasa ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya na kihistoria ndiyo timu ya tatu kwa mafanikio nchini humo; ikiwa imetwaa mataji tisa ya Ligi Kuu, matano ya Kombe la Kagame na matatu ya ndani ya Kenya.

Katika historia yake, Tusker imewahi kutoa wachezaji wazuri wa soka akiwamo MacDonald Mariga wa Inter Milan ya Italia ambaye kwa sasa anachezea Real Sociedad ya Hispania kwa mkopo. Mchezaji mwingine maarufu ni Jacob ‘Ghost’ Mulee.

Kwa sasa timu hiyo ina nyota wengi akiwamo Joseph Shikokoti, mlinzi mrefu wa kati ambaye ametoka kuchaguliwa kuwa mlinzi bora wa Ligi Kuu ya Kenya. Beki huyo amewahi kuichezea Yanga.

Kiingilio katika pambano hilo kitakuwa ni Sh, 2000 kwa mzunguko, Sh 5,000 kwa majukwa ya kawaida na Sh 10,000 kwa wale watakaokaa VIP.

Kiingilio hiki kidogo kimewekwa ili kuwawezesha washabiki wengi zaidi wa soka nchini kupata fursa ya kuona pambano hili ambalo la kirafiki la kimataifa.

"Tunaomba washabiki wajitokeze kwa wingi kuhudhuria pambano hili" amesema Ofisa habari wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga katika taarifa yake aliyotuma kwenye Blogu hii ya Jamii.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages