Breaking News

Your Ad Spot

Feb 3, 2012

ALIYEKUWA REFA WA KIMATAIFA GRATIAN MATOVU AFARIKI DUNIA LEO

Aliyekuwa Refa wa Kimataifa hapa nchini, Gratian Hemans Matovu (pichani), amefariki dunia. jijini Dar es Salaam.

Kwa kujibu wa blogu ya  Daily Mitikasi, Stephen Matovu mtoto wa marehemu, Mzee Matovu amefariki leo majira ya saa 6 mchana, nyumbani kwake Mbezi Beach (Makonde) na taratibu za mazishi zinaendelea hapo hapo nyumbani kwake.

 Mzee Gratian Matovu alianza kuwa refarii wa kimataifa tokea miaka ya 1964 na aliendelea na shughuli hiyo hadi miaka ya 1970 na hadi Mwaka 2006 alikuwa bado katika Kamati ya Marefarii Tanzania.

HISTORIA FUPI
Mzee Matovu alipata Diploma ya Urefarii kunako miaka ya 1956 na akaja kuwa refarii Daraja la Kwanza mnamo Mwaka 1961. Miaka Mitatu baadae alipata Beji ya FIFA.


Mzee Matovu alipata kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Chama cha Marefarii Tanzania.

Kwa Taaria zaidi za wasiliana na STEPHEN MATOVU 0713576666

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages