Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye ndege baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza leo jioni tayari kwa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM yanatofanyika kesho Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
Jk akimsalimia mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikillo
JK akipokea salamu za heshima za Chipukizi wa CCM waliomvalisha skafu baada ya kuwasili
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiongozana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Clement Mabina baada ya kuwasili. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Rais Kikwete akiwasalimia baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege. Anayempa mkono ni diwani katika wilaya ya Geita, ambaye hufahamika zaidi kwa jina la Msukuma
Rais Kikwete akiwasalimia wafanyakazi wa Uhuru FM ambao nao walikuwepo kwenye mapokezi hayo
Rais Kikwete na wenyeji wake wakipata burudani ya ngoma kutoka Ukerewe
Kisha akavutiwa na uchezaji ngoma hiyo na mtoto Nayambani Mganga (3) na kuamua kumtuza fedha
Mvuto wa mtoto huyo ulianza kabla Rais Kikwete hajawasili ambapo Nape naye kwa kuvutiwa naye aliamua kusakata naye ngoma mtoto huyo.
Kisha akambeba na kumchumu kwa upendo na furaha
Akamkumbatia kwa bashasha na hisia kubwa
Hawa ni baadhi wa waandishi wa habari waliofika kwenue mapokezi hayo kwenue Uwanja wa Ndege.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269